Porto na Sporting CP zinakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja kutocheza Ulaya iwapo zitashindwa kulipa madeni ambayo bado haijalipwa kufikia mwisho wa mwezi ujao.

UEFA siku ya Ijumaa ilifichua vikwazo ambavyo vimetolewa kwa vilabu vinane kwa kukiuka kanuni za Financial Fair Play (FFP).
Vinara wa Ligi ya Premeira Liga Porto na Sporting inayoshika nafasi ya pili wametozwa faini ya Euro 300,000 na 250,000 na hawatacheza michuano ya UEFA ya vilabu watakayofuzu katika moja ya misimu mitatu ijayo isipokuwa kama wanaweza kuthibitisha ifikapo Januari 31, 2022 kuwa wamemalizana kulipa “kiasi ambacho kimesalia.”
Klabu ya LaLiga, Real Betis imepigwa faini ya Euro 250,000, huku CSKA Sofia na CD Santa Clara zote zikitakiwa kulipa €75,000 na Mons Calpe SC lazima watoe euro 15,000.
Vilabu vyote hivyo pia vinakabiliwa na kukosa kucheza Europa League katika msimu wa 2022-23, 2023-24 au 2024-25 kama watafuzu, lakini hawajalipa deni.
FC Astana na CFR 1907 Cluj zilitozwa faini ya €150,000 na €200,000, lakini hawakutishiwa kufungiwa.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


