Mbappe na Neymar wangekuwa wafalme wapya? Ulimwengu wa soka umeshuhudia kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 15, hatua za nusu fainali na fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zikichezwa bila uwepo wa Lionel Messi na Christiano Ronaldo!
Kipigo cha aibu, 8-2 cha Bayern Munich kwa Barcelona katika hatua ya robo fainali kilihitimisha safari ya Messi kwenda Lisbon huku safari ya Ronaldo ikitamatishwa na Lyon katika hatua ya 16 tu ya mashindano hayo.
Hii inaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa ufalme ambao Messi na Ronaldo waliuanzisha katika soka la Ulaya. Wengi tulitazamia kuwa ufalme wa wakali hao ungerithiwa na wakali wengine, Mbappe na Neymar! Lakini baada ya mechi ya jana kati ya timu yao PSG na Bayern Munich inabidi tujiulize tena juu ya hili.
Mbappe na Neymar: Wameshindwa Kuifanya PSG Ibebe UEFA Yao ya Kwanza
Wakati Messi akiwa sehemu ya kikosi kilichobeba UEFA mwaka 2006 dhidi ya Arsenal pale Paris, kuwa mchezaji wa muhimu na alieibeba Barcelona katika ushindi dhidi ya Manchester United mwaka 2009 pale Rome huku akiwa na miaka 19 tu, Kylian Mbappe na Neymar wameshindwa kuipa Paris Saint-Germain ubingwa wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa.
Mbappe na Neymar hawakuonesha viwango vya kuridhisha katika fainali hiyo kati yao dhidi ya Bayern Munich, mechi iliyoisha kwa PSG kukubali kipigo cha 1-0!

Wameshindwa Kutumia Nafasi Vizuri
Wote, Mbappe na Neymar walipata nafasi nyingi kipindi cha kwanza ambazo wangezitumia kuongoza mchezo huo lakini hawakufanya hivyo, hata walivyoaminiwa na kocha kuendelea kubaki kipindi cha pili hawakuisaidia timu kusawazisha matokeo kwa timu yao.
Kama Neymar angekua makini, angeiwezesha PSG kupata goli la kuongoza katika dakika ya 18 tu ya mchezo lakini shuti lake dhaifu lilizuiliwa kiurahisi kabisa na Manuel Neuer.
Mbappe nae alipata nafasi adhimu ya kufunga dakika chache kabla ya mapumziko, kocha na benchi zima la ufundi walishasimama kushangilia.
Mashabiki wa PSG kuanzia kule Paris, Lille, Bordeaux na Dar es Salaam, Mbeya mpaka Lindi waliokuwa wanafuatilia mechi kupitia luninga tayari walishaanza kushangili, lakini alichokifanya ni yeye mwenyewe ndo’ anajua! Alichopiga hakina hata hadhi ya kuitwa kijishuti mtoto!
Hata kipindi cha pili baada ya PSG kuwa wanaongozwa kwa goli moja, bado Mbappe na Neymar walishindwa kuonesha ubora wao kuisaidia timu. Dakika za mwisho za mchezo zilishuhudia Neymar akishindwa kufanya maamuzi sahihi akiwa ndani ya eneo la hatari la adui, hakuliona lango wala mwenzie wa kumpasia!
Umri wa Neymar, hapana! Labda Mbappe
Neymar mpaka sasa ana umri wa miaka 28, fainali hii ilikua ni nafasi yake ya pekee kuonesha ubora wake. Kuonesha kwamba anaweza kuwa mrithi wa mmoja kati ya Messi ama Ronaldo. Zaidi kuonesha kuwa anaweza kushinda klabu bingwa nje ya kivuli cha Messi. Kwa kiwango alichokionesha jana, ni wazi kuwa hajayapatia jibu stahili maswali hayo na ubaya ni kuwa tayari anaielekea miaka ya 30s.
Kwa upande wa Kylian Mbappe yeye bado anayo nafasi ya kuwa bora kama magwiji hao, lakini kwa siku ya jana bado hakufanya hivyo. Labda anaweza kusingizia kuwa alitoka kwenye majeraha ya enka, lakini asisahau kuwa alicheza katika mchezo wa nusu fainali! Mbappe hivi sasa ana miaka 21, bado ana miaka mingi ya kucheza, labda huko mbeleni anaweza kututhibitishia kuwa yeye ni bora kama Messi ama Ronaldo, lakini kwa jana HAPANA!
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


warda
Jamani Mie imeniuma sana PSG kukosa Huu Ubigwa
felister
neymar na mbappe hawawezi kua Kama Messi na Ronaldo labda uko mbeleni
Adelta
Viwango vyao bado hawawezi kumfikia Messi@meridianbettz
magdalena
neymar na mbappe wafanye kazi ya ziada mpaka kuwafikia hao
rama
Maoni:kwel kabisa japokuwa messi na ronaldo ushindani wao umepungua sana tangu ronaldo haondoke kwenda juve
Mwanahamisi
Bora ajitaidi kuongeza bidii ili amfikie messi
Tatu
Kila MTU Jana aliona kabisa huu ushindi wa PSG lakini imekuja kutokea tofauti pale mbappe na neymar alivokuja kucheza vibaya uwanjani na kuzidiwa uwezo na kijana mdogo sana aitwae kingsley coman
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli Neymar na mbappe awawez kuwa Kama Messi Ila kwakizidisha juhudi Wana weza wakawa kwenye levo ya Messi Ila wakaze tuu Ila Messi ana mpinzani wakae wakijua Messi yupo vizuri
Khadija
hata wafanyeje hawawezi kimfikia#meridianbettz
aisha
Messi kile ni kifaa kingine usikifananishe na mtu mwingine
Salma ngende
Awawez kufanana na wengine
Furahav
Hawana uwezo wa kuwafikia messi na Ronaldo.
Saupha mohamed
Kuwafikia mess na Ronaldo wafaye kazi kweli kweli
Issa
Ni wachezaj wazuri sema hawana umakini pia hicho ndio kinawafanya wasifikie levo za mess na ronaldo kwa chans kama zile walizopata na kwa mechi kama ile sidhani kama angeluw mess ama cr7 wangefanya ajiz
Ernest
Huu ni ukweli usiofichika kuwa Messi na CR7 ni watu wa level nyingine kabisa dhidi ya Mbappe na Neymar, Messi na CR7 wataendelea kutamba kwenye kizazi hiki adi watakapoacha soka la kulipwa
Sadick
Record za Messi na Ronaldo sio rahisi kufikiwa na yeyote kwasasa kwa namna walivyo na shauku ya kupata mafanikio zaidi na zaidi. Jana Neymar na Mbappe haikuwa siku yao#meridianbettz
felister
neymar na mbappe hawawezi kua Kama Messi na Ronaldo labda uko mbeleni
Fatuma kasomo
Habari njema
Theckla
Yuko sahihi
Povel
Hayo maneno tu kwn wakiongezeha bidii na kujituma wanawez fika malengo hakuna kukata tamaa kwny kutafuta maisha
Hope mwaikuka
Wamefanya kwa nafas zao ila ndo hvyo lazma tukubaliane na kilichotokea
Rose kapinga
Messi na ronaldo izo level nyingine wapambane xana!!!
Amiri Kayera
Kufk level iz ngum san
Sabrina
Duuh Huo nie ukweli usio pingika hauwezi kuwafananisha kabisaa
jullie
wanaweza wajipange upya
Shafii
Messi na ronaldo ni mpango mwengine cha msingi mbape na neymar huu ndo wakati wao kwa sababu messi na ronaldo zama zao zinaenda ukingoni.
Latifa juma mohamed
Hayo maneno tu kwn wakiongeza bidii na kujituma wanawez fika malengo hakuna kukata tamaa kwny kutafuta maisha , siku zote mtafutaji hachoki
David Pere
Messi na ronaldo ni mpango mwengine cha msingi mbape na neymar huu ndo wakati wao kwa sababu messi na ronaldo zama zao zinaenda ukingoni.
farida ahmadi
Kweli kabisah ila wasikate tamaa waendelee kukaza buti neymar na mbape
Rehema
Neymar akaze buti
Dorophina
Kila jambo linawezekana wakiamua kwani hao Messi na Ronaldo wamefanyaje mpaka wamefika hapo walipo
Sauda
Wapambane, wataweza
Tahiya
Ni suala la kuwap muda tyuu vijana wakali
Zeiyana
Tatizo lake mbappe alikua na shauku sana ..!nia yake yeye kuipelekea clabu yake kufuzu ubingwa balani ulaya ili kutimiza ndoto yake alijisahau kama watu mwenyew wanao kutana nao si wamchezo mchezo..!ila sio mbaya bado hana nafasi kubwa tu hajipange asikate tamaa..!
Caroline
Messi na Ronaldo watabaki kua juuuuu
Nasra
Nawakubali wote
Samiah
Yuko sahihi
Ester jackson
Wanaweza mana tunaona walivyo onyesha uwezo wao msimu huu kama wataweza kuongeza juhudi wataweza kuwapita kabisa
Fatina mfingi
Wote noma!!