Kingsley Coman: Mfalme wa Lisbon

Wamezoea kumuita ‘The King’ wanapokuwa mazoezi. Katika kudhihirisha ufalme wake, Kingsley Coman akawatoa machozi Neymar na Mbappe.

Mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa – UEFA kati ya PSG na Bayern Munich uligubikwa na majina ya mastaa wa PSG , Neymar na Mbappe. Ila kama ilivyokawaida, mpira unadunda dakika 90. Haikuwa Lewandowski wala nyota wa PSG ambao wamefanya usiku uwe wa aina yake ila ni Kingsley Coman – The King

Katika badiliko pekee kwenye kikosi cha Hans Flick, Coman alichukua nafasi ya Ivan Perisic kama winga wa kushoto. Goli lake la kichwa lilitosha kupeleka shangwe Ujerumani na kuwaacha Ufaransa wakitoa machozi.

Kingsley Coman (kushoto) akishangilia goli lake. Neymar (kulia) akimwaga machozi.
Kingsley Coman shujaa wa Bayern Munich.

“Nina furaha isiyokifani lakini pia ninawahurumia PSG. Inaniuma kidogo japokuwa mimi ni Bayern 100%” amesema Kingsley Coman.

“Pengine msimu huu [Coman] ametoka kwenye vivuli vya Ribery na Robben. Ana kipaji cha hali ya juu na amekionesha leo, anaweza kufunga magoli.” amesema Hans Flick.

“Kwa yeye kufunga lile goli baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu, ni jambo la faraja kubwa” amesema Serge Gnabry.

“Tulikuwa tunafikiria mabadiliko mawili ambayo pengine Bayern wangeyafanya, lakini tulishangazwa kuona Coman ameanza. Perisic alifanya vizuri kwenye michezo yao iliyopita, kulikuwa na kasi kubwa na kutumia muda mwingi kujilinda.” amesema kocha wa PSG – Thomas Tuchel.

Ramani ya mipira aliyogusa Kingsley Coman kwenye mchezo wa fainali.

Coman aligusa mpira mara 38 na kumpatia wakati mgumu beki wa kulia wa PSG – Thilo Kehrer. Muda wake wa kufanya maajabu ulionekana kipindi cha pili baada ya kupachika goli na kumfanya kuwa Mfaransa wa 5 kufunga goli kwenye Fainali ya UEFA na wa kwanza kufunga goli dhidi ya timu ya Ufaransa.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

36 Komentara

    Kwa kweli Coman anastahil kuwa mfalme#Meridianbettz

    Jibu

    kwa yeye kufunga lile goli baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu ni jambo kubwa

    Jibu

    Maoni:hongela sana bayern kwa ubingwa mumekuwa na kikosi bora sana msimu huuu

    Jibu

    Coman Yuko vizuri anastahili kuitwa mfalme@meridianbettz

    Jibu

    Coman Yuko vizuri

    Jibu

    lile goal alilopiga lilikuwa balaa ata psg hawakulitegemea

    Jibu

    King coman watoa machozi neymar na mbappe tatizo PSG walijiamini sana walikuwa ajui kama mpira unadunda na matokeo dk 90 walichokitaka wamekipata hongera bayern

    Jibu

    Kiukweli Coman Anajua yupo vizuri kwenye kaz yake anastairi pongez

    Jibu

    comani yupo vizuri#meridianbettz

    Jibu

    Comani anajua sana namkubali mnoo

    Jibu

    Anastahili ilo

    Jibu

    Namkubali sana coman.

    Jibu

    Coman yupi vizuri

    Jibu

    Coman alifanya jambo sahihi na kwa wakt sahihi bayern walistahili

    Jibu

    Kingsley Coman ni hazina kubwa sana kweli ulimwengu wa soka na kama bado ataendelea kuwepo kwenye ubora wake basi tutegemee makubwa kutoka kwake

    Jibu

    Hii gemu kiukwel ilikuwa ngumu sana kutabirika maana timu zote zilijipanga kimashindano

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Congrat Kingsley COMAN man of the man Usiku wa fainal ya ligi ya Mabingwa ulaya

    Jibu

    Gud to him

    Jibu

    Huy nd alipelek kilio Kwa psg

    Jibu

    Coman mahiri xana!!!

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Yani roho imeniuma sana PSG kukosa ubingwa wamechana mkeka wangu.

    Jibu

    Kuna msemo unasema yaliyomo yamo hili lili jionesha kabla ya mechi kwamba Bayern ndio bingwa kwa hali yeyote ile.

    Jibu

    Yupo vizur

    Jibu

    Coman Yuko vizuri anastahili kuitwa mfalme@meridianbettz

    Jibu

    Hii gemu kiukwel ilikuwa ngumu sana kutabirika maana timu zote zilijipanga kimashindano

    Jibu

    Hanaweza pia na hanajua coman ni mchezaji mzuri Sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Coman is talent player

    Jibu

    Anastahili kuwa mfalme

    Jibu

    PSG wanaweza kumuita Coman ndio mchawi wao..!hawaamini walicho kiona

    Jibu

    Coman kweli ni.THE KING

    Jibu

    Anastahili haswaa

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.