Messi: Inter Miami Itakua Klabu Yangu ya Mwisho

Staa wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye kwasasa anakipiga ndani ya klabu ya Inter Miami amesema kua anafikiri klabu hiyo ambayo inashiriki ligi kuu ya Marekani maarufu kama (MLS) ndio itakua klabu yake ya mwisho kuitumikia.

Messi ameweka wazi kufikia sasa anajiona kabisa Inter Miami itakua klabu yake ya mwisho na hii ni baada ya kuzitumikia klabu ya Barcelona kwa muda mrefu, Lakini pia klabu ya soka ya PSG kutoka nchini Ufaransa ambayo ameitumikia kwa takribani misimu miwili.MessiStaa huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona kwasasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Argentina akijiandaa na michuano ya Copa America ambapo wao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo alisema hivi “Napenda kucheza mpira, nafurahi kila kitu zaidi kwa sababu najua kila mara kuna mengi zaidi yanayopungua”

Messi ameonesha kua anatambua kadri siku zinavyoenda mbele makali yanapungua hivo anaamini kua umefika wakati wa yeye kupumzika licha ya kua anaupenda sana mchezo wa mpira wa miguu, Lakini anatambua kila lenye mwanzo halikosi mwisho ndio sababu ya yeye kuona Inter Miami itakua timu yake ya mwisho kuitumikia.

Acha ujumbe