Messi: Nilijisikia Vibaya Sana Msimu wa Joto

Huu ukiwa ni msimu mgumu sana katika historia yake ya kuwepo Barcelona, tangia sakata lile la uhamisho la kiangazi, Lionel Messi anasema kuwa ameamua “Kupambania kila kitu” huko Barcelona msimu huu.

Fowadi huyo wa Argentina alifikisha rekodi ya Pele ya mabao 643 kwa klabu moja na ana nafasi ya kuvunja rekodi tena kwa kuandika rekodi ya peke yake wakati Barcelona inakabiliana na Real Valladolid Jumanne, na kumzidi mtangulizi wake Pele.

Messi, ambaye alikuwa karibu na kuondoka Barcelona mnamo Agosti wakati wa sintofahamu baina yake na uongozi wa kilabu, anasema ameongeza tena umakini kwa msimu uliosalia.

Laporta: Nikishinda Urais Nitambakisha Messi Barcelona.

“Ukweli ni leo mimi naisikia vizuri, lakini nilikuwa najisikia vibaya wakati wote wa majira ya joto, kabla ya majira ya joto, kwa sababu ya jinsi msimu ulivyomalizika,” alinukuliwa akizungumza na kituo cha Televisheni cha Uhispania La Sexta.

“Ndipo ikaja kile kilichotokea wakati wa kiangazi, burofax na yote hayo kwa pamoja. Halafu kisha nikaanza nayo mwanzoni mwa msimu. Siku hizi, najisikia vizuri.”

Messi amesema bado hajapoteza muelekeo na Barcelona na anaziingatia kile kinachotegemewa kutoka kwake, anajiona bado ana ari ya kufanya vyema licha ya yale yaliyotokea na ukweli kuwa klabu inapitia kipindi kigumu.


 

VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

12 Komentara

    Habari njema

    Jibu

    Mess anabak jina mpira umeisha

    Jibu

    Messi Bado yupo vizuri ma anazidi kuwa
    Karibu na Barcelona

    Jibu

    Uyo ndo Messi

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Messi Bado Yuko vizuli

    Jibu

    Uamuz mzur messi

    Jibu

    Messi yupo vizuri

    Jibu

    Messi kama messi

    Jibu

    Messi yuko vizuri

    Jibu

    Nikweli lazima usiwe poa Jembe zote nichangamoto zakwenye soka

    Jibu

    Hata mie kama Messi msimu wa joto najisikiaga vibaya sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.