Michael Sarpong, Mshambuliaji wa kikosi cha Yanga raia wa Ghana amepitisha jumla ya siku 170 ambazo ni sawa na saa 4,080Â bila kufunga bao kwenye mechi zote za ushindani ikiwa ni zile za Ligi Kuu Bara na Shirikisho.
Kwenye Ligi Yanga ina pointi 61 baada ya kucheza mechi 29 na ina mabao 43 amehusika katika mabao 7, alifunga mabao manne, pasi mbili za mabao na alisababisha penalti moja kwenye mchezo dhidi ya KMC, Uwanja wa CCM Kirumba.
Bao lake la kwanza ndani ya Ligi alifunga Uwanja wa Mkapa kwenye sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, ni Septemba 6 kisha Oktoba 31 aliwafunga Biashara United, Uwanja wa Karume.
Novemba 7, Sarpong aliwafunga Simba ilikuwa ni kwa mkwaju wa penalti na Desemba 6 alifunga akaunti yake ya mabao kwa kuwafunga Ruvu Shooting ilikuwa Uwanja wa Mkapa.
Leo Mei 25 anatarajiwa kuongoza kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC ikiwa ni hatua ya robo fainali.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kambarage majira ya saa 10:00 jioni na mshindi wa jumla atainga hatua ya nusu fainali ambapo atakutana na Biashara United aliyeshinda mbele ya Namungo FC.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Asante kwa taarifa