Inaendelea….
Kuwepo ndani ya kuta za gereza kwa mara 38 katika umri wa miaka 13 ni matunda ya maisha korofi aliyojilea mwenyewe Mike Tyson.
Baba yake aliitosa familia yao akiwa na miaka 2 tu. Mama yake aliachiwa msalaba wa kulea watoto watatu peke yake.
Mama yake alifariki Tyson akiwa na miaka 16, kisha dada yake akafariki Tyson akiwa kijana wa miaka 24. Kifo cha mama yake kilichangia sana kuathirika kwa maisha ya Tyson. Tyson aliwahi kusema,

“Sikuwahi kumuona mama yangu akiwa na furaha au kujivunia mimi kama mwanae, alinijua tu mimi ni mtoto mkorofi ninayepigana hovyo mitaani.
Alizoea kuniona nikirudi nyumbani na nguo mpya ambazo alijua sijazilipia. Inaniuma sana kwasababu hajawahi kuniona akafurahi kwa ajili yangu”
Ni maisha haya ya kikorofi yalimfanya Mike Tyson ajitafutie usalama, alijua kifo hakipo mbali na yeye, akaamua kujiimarisha kwa kupigana ngumi za mtaani.
Mkasa wake wa kuingia kwenye boxing ulianza asubuhi moja akiwa sero, alipokutana na bondia wa zamani Bobby Stewart aliyeyatazama maisha yake na kuona hasira na utukutu wa Tyson unaweza kutisha sana ulingoni.

Huyu Stewart ndiye aliyemfundisha boxing na kumkutanisha na Cus D’Amato. Baada ya hapo ilifuata historia na ukale wake.

Katika umri wa miaka 21 alishaitwa ‘The baddest man on the planet’. Alishashinda mapambano yake 34 kati ya 34, ‘mind you’ 31 aliyamaliza kwa KO.
Alikuwa na kauli mbiu moja tu ulingoni, ‘I either kill you or you kill me‘. Tyson alilitazama pambano kama vita, kichwa chake ulingoni kilimuambia ‘Upo hapa kwa ajili ya kuua na si vinginevyo’.
Maisha yake yalitaliwa na ukatili na ukorofi mwingi nje ya ulingo. Kipo kipindi alihukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa ubakaji. Ukatili aliubeba hadi nje ya ulingo.
Siku moja akizungumzia maisha yake nje ya ulingo, Tyson alikubali kweli hakuwa binadamu mwema nje ya ulingo lakini tatizo ni kwamba dunia inamtazama zaidi kama shetani, wakati kuna muda alikuwa malaika nuru.
Tyson anadai binadamu wanamuandika tu kwa mabaya wakati amefanya mambo mengi mema. “Hata kama sijafanya wema hata mmoja, basi heshimuni nilichoufanyia mchezo”.
Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx
Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.
Legend wa ukweli sio wa kuchonga
Yupo vizuri
Nmemuelewa
Tyson natamani enzi zake zirudi