Barcelona Kumkosa Suarez ni Kama Madrid Kumkosa Ronaldo

Msimu wa kwanza kwa Barcelona bila mshambuliaji Luis Suarez umelinganishwa na Real Madrid ambao wamekuwa wakipambana sana baada ya kuondoka kwa mshambuliaji Christiano Ronaldo ambaye alitimkia katika ligi ya Serie A, amesema Diego Forlan.

Barcelona Kumkosa Suarez ni Kama Madrid Kumkosa Ronaldo

Mchezaji wa zamani wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Uruguay pia anaamini maamuzi ya Barca kumuuza Suarez yalikuwa hayana mantiki kutokana na kiwango chake uwanjani.

Barca wapo nyuma ya Atletico Madrid katika jedwali la LaLiga kwa tofauti ya alama tano, wakati ni Lionel Messi pekee ambaye amefunga mabao mengi zaidi kuliko Suarez msimu huu.

Juu ya Kumuuza Suarez, Forlan aliiambia AFP: “Ni kweli lilikuwa kosa kubwa sana, waliposema sema Suarez yupo sokoni, nilijua lilikuwa ni kosa.

“Ninachokijua lilikuwa siyo swala la kiwango chake uwanjani.

“Barcelona wanamkubuka Suarez kama Ronaldo alipoondoka Real Madrid,” Forlan alisema.

“Halikuwa jambo la Ronaldo kuondoka, moja ya wachezaji bora katika historia ya mpira wa miguu, ni magoli 50 yalikuwa yameondoka.

“Kwa hiyo ukiuza wachezaji kama Ronaldo au Suarez, unapaswa kupata mbadala wao wenye kiwango kama kile kile pia ni kuhatarisha maana inabidi wapte muda wa kuzoea mazingira.

“Ronaldo alipoondoka mambo yamekuwa magumu kwa Real Madrid na kwa Upande wa Barcelona sasa imekuwa hivyo hivyo.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

  CHEZA HAPA

9 Komentara

    Nadhani ilifika mahali aondoke Barcelona na kupisha wengine. Na pengine Koeman hakumpenda

    Jibu

    Barcelona yupo sahii

    Jibu

    Luis ni mshambuliaji bora

    Jibu

    Sidhan kama ni kwel

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Kazi kweli kweli

    Jibu

    Duuh hiyo kazi

    Jibu

    Duu kaz kweli

    Jibu

    Kabisa

    Jibu

Acha ujumbe