Klabu ya AC Milan iliyopo chini ya kocha mkuu Stefano Pioli wanakabiliwa na tatizo kubwa la majeruhi kuelekea mechi kubwa dhidi ya Chelsea na Juventus, huku taarifa zikisema kuwa wanaweza kuwa na wachezaji pungufu zaidi ambao watakuwa wanapatikana siku ya Jumatano kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.
The Rossoneri walipambana na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 wakiwa ugenini dhidi ya Empoli jana usiku, mchezo ambao ulikuwa na mabao matatu yaliyofungwa dakika ya 90 na vilabu hivyo viwili.
Pia ilishuhudia Davide Calabria akitolewa nje kwa machela kutokana na kushukiwa kuwa na msuli wa paja ambao ungeweza kumuweka nje hadi baada ya mapumziko ya Kombe la Dunia, wakati Simon Kjaer alikuwa na tatizo la paja la kulia na Alexis Saelemaekers aliteguka goti.
Hilo ndilo jambo la mwisho ambalo kocha Stefano Pioli alihitaji, kwani tayari alikuwa akiwakosa Mike Maignan, Junior Messias na Theo Hernandez, Divock Origi, Zlatan Ibrahimovic na Alessandro Florenzi.
Tatizo katika Ligi ya Mabingwa linachangiwa na ukweli kwamba Milan wana orodha ndogo ya kikosi kutokana na ukosefu wa wachezaji wa Italia na wazawa. Walilazimika kuwaacha Ciprian Tatarusanu, Aster Vranckx, Malick Thiaw, Yacine Adli, Tiemoue Bakayoko na Ibrahimovic.
Hivyo basi hii inamaanisha kuwa Milan inapaswa kwenda London siku ya Jumatano ikiwa na wachezaji 14-15 tu wa nje wanaopatikana