Modric Atamani Uwepo Wa Mashabiki Anfield

Kiungo wa Real Madrid Luca Modric anahisi ni bora sana akutane na Liverpool pale Anfield kukiwa na mashabiki, ambao huleta hali ya hamasa na kuongeza upinzani.

Kiungo huyo wa Madrid alifanikiwa kucheza Anfield akiwa na Tottenham katika Premier League na akiwa na Real Madrid pia alicheza hapo katika michuano ya UEFA.

Modric anaamini kwamba licha ya wao kuwa ugenini, mashabiki wanaongoza hamasa sana kwa wao kama wachezaji kutamani kuonesha ujuzi zaidi.

Real Madrid watakutana na Liverpool kati mkondo wa pili wa robo fainali ya UEFA pale Anfield siku ya leo majira ya saa nne usiku, huku wakiwa na kumbukumbu nzuri za kushinda magoli 3-1 wakiwa nyumbani. 

Katika mechi hiyo Liverpool watalazimika kushinda magoli mawili bila au magoli zaidi ya mawili bila kuruhusu washambuliaji wa Madrid kugusa nyavu zao. Liverpool watawakosa nyota wao wa muda mrefu Virgil Van Dijk na Henderson huku Curtis Jones anategemewa kurudi baada ya kupona majeraha ya misuli.

Real Madrid wataendelea kuwakosa nyota wao Sergio Ramos, Raphael Varane, Eden Hazard na Carvajal ambao wana majeraha na kukutwa na COVID-19. Kocha wa Madrid anaamini kwamba kukosekana kwa wachezaji wao hakupaswi kuonekana kama udhaifu kwani wapo vizuri sana na wamejiandaa kushinda mechi hiyo.

“Hii itakuwa ni mechi ngumu sana kwetu, lakini tumejiandaa vyema licha ya kuwa na wachezaji ila waliokuwepo ni bora pia….. Kiukweli natamani uwepo wa mashabiki kwani wanaongeza hamasa ya uchezaji” alisema Modric katika Tweeter yake.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Kweli kabisa mashabiki ni kila kitu

    Jibu

    Ila kwel

    Jibu

    Mpira raha uwe na mashabiki

    Jibu

Acha ujumbe