Kiungo fundi wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Crotia Luca Modric ametimiza mechi ya 450 klabuni dhidi ya klabu ya Sevilla jana usiku katika mchezo waliokua nyumbani katika dimba la Santiago Bernabeu.modricKiungo huyo alikabidhiwa jezi na rais wa klabu hiyo Florentino Perez yenye namba 450 ikimaanisha kiungo huyo gwiji katimiza idadi ya michezo hiyo akiwa klabuni hapo ambapo alijiunga majira ya joto mwaka 2013.

Hafla hiyo ilifanyika kabla ya mchezo dhidi ya Sevilla ambapo Real Madrid walishinda mabao matatu kwa moja huku Modric akiwa ni miongoni mwa wfungaji wa mabao katika mchezo.Kiungo huyo ambaye alivalia kitambaa cha unahodha usiku huo akiwa na kiwango bora kabisa amefanikiwa kuingia kwenye rekodi za miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo walioitumikia klabu hiyo michezo mingi.modricLuca Modric ni miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa kwa kiwango kikubwa klabuni hapo huku akikumbukwa zaidi kwenye utatu walioutengeneza klabuni hapo kwenye eneo la katikati akisaidiana na Toni Kroos pamoja na Carlos Casemiro alietimkia Manchester United na kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa