Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison leo ameanza safari kuelekea Bukoba kuungana na wachezaji wenzake ambao wana mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Julai 8.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, kwa kufungwa mabao 3-0, utapigwa Uwanja wa Kaitaba.


Jana, Julai 5 wakati Yanga ikilazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United ilikosa huduma ya Morrison ambaye aliachwa Dar.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alisema kuwa iwapo atamhitaji Morrison kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar atawaambia viongozi wampeleke.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram Morrison amewaambia mashabiki wake kuwa habari Bukoba, niambieni kile ambacho sijaskia.

Morrison amefunga jumla ya mabao matatu na kutoa pasi tatu ndani ya Ligi Kuu Bara.

48 MAONI

  1. Drama za Morison hazileti afya ya soka letu. Kama mchezaji ana mkataba na timu ni lazima aheshimu hilo bila kubembelezana kama hili la Morrison#meridianbettz

  2. Pamoja na kuwafuata Yanga Bukoba ,Morrison anawachanganya sijui amegundua wanamuhitaji sana, maana yake kama timu zetu anazipima akili ila na timu zenyewe bado hawajielewi .

  3. Morison n mchezaj mzr sema sasa naona anapagawa na kelele na ushawishi wa timu pinzani ndio tabu ya wachezaji wa kigen wanapenda kusujudiwa wakiona timu kadhaa kubwa na vyombo.vya habar zikimzungumzia yeye ana jiona ndio mfalme inabidi waheshimu mikataba na sheria za club #meridianbet

  4. Morrison anazingua sana na tatzo viongozi wake wanalea Sana Ayo mambo ndo maama heshima katika timu anakuwa Hana anafanya anavyotaka yeye

  5. Morrison anayumba Bado ajakielewa Nini anakifanya mchezaji anahejielea Hawez kukaa sehemu bila usajili izo no drama anatuchezea huyo

  6. Morrison yupo poa ila anahitaji matunzo pale yanga ili asiweze kutoka hapo yanga,jamaa anajua sana na hana mbadala pale yanga ndio maana analinga sana

  7. Morrison ni jembe, vema akienda huko inawwsekan yanga wakafanya vzr Zaid maan young African Hali c poa wananiboa tu wanapoanza kutangulia kwa magoli halafu wanaishia njian nenda baba okoa jahaz.

  8. Yani hapo ulw msemo hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu umeaminiwa na morison mwenyewe kakubali yaishee

  9. Ni jambo zuri kwa wana yanga kuongeza nguvu kwenye kikosi kwani tunafahamu kua Morison ni mchezaji mzuri na mzoefu.

  10. Morrison ni mchezaji mzuri sana kwa timu ya yanga lakini kwa mchezaji huyu namuona kama anajitenga kutokana na ujuaji wake wa Mpira au vishawishi kutoka kwa timu pizani mana amejiweka nyuma sana kuacha na timu Mara nyingine hivyo sijui kwa sababu gani hili linatokea kwake tu na isiwe wengine kama ingekuwa kwa nchi nyingine angeshapigwa faini au kufungiwa kushiriki katika timu kadhaa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa