Nyota wa Man United Nemanja Matic amesaini mkataba mpya kuendelea kusalia klabuni hapo. Mkataba wa sasa unamfanya aendelee kuweko klabuni hapo hadi mwaka 2023.

Staa huyu, ambaye ni raia wa Serbia alikuwa amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa awali. Lakini Jumatatu hii, nyota huyu amemwaga wino kwenye masharti mapya ya mkataba baada ya kuonekana kufanya vyema pale Old Traford chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

Matic ana umri wa miaka 31 sasa, na alijiunga na Man United akitokea Chelsea mwaka 2017. Mpaka sasa nyota huyu amecheza jumla ya mechi 114. Ana matarajio ya kucheza mechi nyingi zaidi chini ya Solsjaer.

Nemanja Matic Ameongeza Dili la Miaka 3
Nemanja Matic

Matic anasema anafurahia sana kuwepo United, na anafurahia zaidi kuona kuwa ataendelea kuwepo hapo kwa kipindi kingine tena kijacho.

“Nina furaha sana kuwa nitaendelea kuwa sehemu ya klabu hii, kama mchezaji bado nina mengi zaidi ya kufanya kwenye soka langu la kulipwa, na kufanya hivyo na Manchester United ni heshima kubwa.” -Nemanja Matic

Solskjaer anasema amefurahi sana staa huyu kusaini mkataba mpya, anaamini staa huyu atakuwa mfano kikosini. Hii ni kutokana na uzoefu wake katika soka la kulipwa.

 


 

Unajua kuwa Meridianbet wanatoa mizunguko 50 ya bure kwa mteja mpya? Jisajili sasa na ufurahie burudani na ushindi wa Kasino ya Mtandaoni.

JISAJILI HAPA

Mizunguko ya Bure | Kasino ya Mtandaoni

 

54 MAONI

  1. Matic yupo poa sana na anafanya vizuri sana kuongeza mkataba hapo O.T ni jambo zuri sana acha aendelee kukipiga nachini ya kocha wake nyota wa zamani wa Manchester United ole Gunnar

  2. Nyongeza ya miaka 3 kwa Matic mwenye miaka 31 ni kubwa mno. Katika umri huo wachezaji wengi hukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara tena kwenye nafasi ya kiungo ya kutumia nguvu#meridianbettz

  3. Kwenye timu unapohitaji kua mshindani ni lazima kikosi chako kiwe kipana na chenye kuhitaji aina Fulani ya mafanikio kwa walicho kifanya man u ni jambo zuri kwani matic atakua msaada hasa kwenye sehemu ya kiungo kwani bado yuko vizuri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa