Newcastle United walikuwa wanahusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial. Taarifa zinataja kuwa klabu hiyo haina mpango wa kuendelea kuiwinda saini ya staa huyu.
Kwa mujibu wa wakala wa staa huyu, Martial anatamani sana kuondoka Man United kwenye dirisha la uhamisho la mwezi Januari kutokana na kukosa muda wa kutosha wa kucheza.

Klabu ya Newcastle United ilitajwa kuwa kwenye mpango wa kuinasa saini ya Anthony Martial, wakati mmiliki mpya wa klabu hiyo akijaribu kuwekeza pesa zaidi kuinusuru klabu hii katika kushuka daraja msimu huu.
Lakini kwa mujibu wa Footbal Insider staa huyu siyo kipaumbele cha Eddie Howe, hivyo Newcastle wameamua kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha saini yake.
Sababu nyingine inayotajwa kuchangia kukwamisha zoezi la kujaribu kumsaini staa huyu ni mshahara wa £240k kwa wiki ambao Martial analipwa kwa sasa. lakini Newcastle bado wana matumaini ya kuboresha kikosi na kujinusuru kushuka daraja.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


