Nicolò Zaniolo Athibitisha Kuikosa Euro 2020

Nicolò Zaniolo ameweka wazi kuwa hataweza kushiriki Euro 2020, lakini atakuwa anajiandaa kushiriki Kombe la Dunia.

Nyota huyu wa timu ya taifa ya Italia, na klabu ya Roma alipata changamoto ya majeraha mwaka 2020, jeraha la mwisho alilipata kwenye mechi kati ya Italia na Netherlands mwezi Septemba.

Zaniolo alikuwa anatarajiwa kurejea dimbani mwezi huu wa Aprili, lakini baada ya kutembelewa na profesa Fink pale Innsbruck, alishauriwa kusubiri kidogo, hivyo hataweza kurejea  dimbani mapema Aprili.

Nicolò Zaniolo Athibitisha Kuikosa Euro 2020

Kwa mujibu La Gazzetta dello Sport, Zaniolo anahitaji mda kidogo kwa ajili ya misuri yake kuimarika zaidi. Hivyo, kuepuka changamoto yeyote ambayo inaweza kujitokeza, Zaniolo anahitaji kusubiri.

“Sijafurahia, lakini niko tayari kwa ajili ya kushiriki Kombe la Dunia mwakani.” Nicolo mesema akizungumza na La Gazzetta dello Sport.

Kocha wa Italia pia amesisitiza kuwa wanatambua kuwa hawawezi kuwa na Nicolo kwa sasa, ila anapaswa kuwa mvumilivu akisubiri mambo kuwa sawa.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Vizuri Sana

    Jibu

    Majanga

    Jibu

    Itakuwa poa

    Jibu

Acha ujumbe