Nyota wa Liverpool, Naby Keita Akwama Guinea

Liverpool wameridhishwa na hali ya usalama wa nyota wao Naby Keita huko Guinea, baada ya mapinduzi ya serikali nchini humo.

Taarifa zinasema kuwa klabu hiyo kwa sasa inafanya mazungumzo na mamlaka zinazohuisika kuhakikisha wanamrejesha nyota huyo akiwa salama.

Nyota huyu alirejea nchini kwake kwa ajili ya majukumu ya kitaifa na timu yake ya taifa kabla ya tukio la kumpindua Alpha Conde.

Naby Keita Akwama Guinea
Naby Keita

Kupinduliwa kijeshi kwa serikali ya Alpha Conde kulionesha wasi wasi wa hali ya usalama nchini humo, huku kukiripotiwa majibizano ya risasi kwa saa kadhaa katika maeneo ya ikulu na pande zinazotajwa kuwa wanajeshi waliokuwa na nia ya kumuondoa raisi huyo madarakani, na walinzi ambao wana utii kwa raisi huyu.

Sakata zima la kupinduliwa kwa raisi huko Guinea, imepelekea kuahilishwa kwa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.

“Tuna mawasiliano ya mara kwa mara na Naby Keita, pamoja na uongozi wa timu yake ya taifa. Tunafurahi yupo salama na anahudumiwa vizuri. Hali siyo nzuri sana tunajitahidi kuhakikisha anarejea Liverpool.”

– Msemaji wa Liverpool.


 

USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

INGIA MCHEZONI HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.