Cristiano Ronaldo Aweka Rekodi Duniani.

Moja kati ya kauli ambazo ziliwahi kunukuliwa kutoka kwa Cristiano Ronaldo ni “sizitafuti rekodi, rekodi zinanitafuta mimi” hakika, rekodi za CR7 ni nyingi mno.

Kwa takribani wiki 2, CR7 ameviteka vichwa vya habari ulimwenguni. Alianza kwa kuomba kukaa benchi kwenye mchezo wa Juventus vs Udinese, muda mfupi baadae, ikaripotiwa kuwa alimuhakikishia Maximiliano Allegri kuwa angesalia Juve. Fumba kufumbua, CR7 akahusishwa na kutimkia Man City, dakika chache akaonekana akiondoka viwanja vya mazoezi vya Juventus na paap!!! Ndani ya saa 2, usajili wa Cristiano Ronaldo kurudi Man United ukatangazwa rasmi.

Wakati mashabiki wa United na wadau wa soka wakiendelea kuongelea kurejea kwa Cristinao Ronaldo pale Old Trafford, mchezaji huyu akiwa na umri wa miaka 36 kwa sasa, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi (111) ya timu ya Taifa. Hii ni baada ya kupachika magoli 2 kwenye mchezo kati ya Ureno vs Ireland na kuivunja rekodi ya Ali Daei (109).

CR7 akishangilia rekodi yake ya Dunia,

Sasa ni hivi, muda mfupi baada ya kuthibitishwa kuwa Cristiano Ronaldo atavaa jezi namba 7 akiwa na Man United kwa mara ya pili, mauzo ya jezi hiyo yameweka rekodi ya kuwa jezi (ya timu 1) iliyouzwa kwa wingi zaidi (mtandaoni) duniani ndani ya saa 24.

Hii ni rekodi ambayo CR7 anaivunja rasmi rekodi aliyokuwa anaishikilia Lionel Messi (alipojiunga na PSG), Bryce Harper (aliposajiliwa Philadelphia Phillies), Tom Brady (alipojiunga na Tampa Bay Buccaneers) na LeBron James (alipojiunga na LA Lakers).


USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

INGIA MCHEZONI HAPA

Acha ujumbe