Bernabeu Mpya, Real Madrid Mpya

Licha ya kumkosa Kylian Mbappe katika dirisha lililopita la usjaili Real Madrid haijakata tamaa bado wapo kwenye mipango ya kumleta Bernabeu mshambuliaji huyo wa Ufaransa ambaye mkataba wake na PSG utafika tamati mwaka ujao hivyo ataondoka kama mchezaji huru.
Bernabeu Mpya, Real Madrid Mpya
Uwanja mpya wa Santiago Bernabeu

Mjenzi wa uwanja mpya wa Real Madrid Estadio Santiago Bernabeu, ambao bado upo kwenye ujenzi unabadilishwa wakati bado unabaki na alama ile ile.

Dimbani kuna marekebisho ya mradi na inafanyiwa kazi katika kikosi cha wakubwa baada ya kuondoka kwa Sergio Ramos na Raphael Varane hivyo wamesajili wachezaji amabao wanatazamiwa kukidhi haja ya mwalimu katika safu ya Ulinzi kwa kuwasajili David Alaba na Eduardo Camavinga.

Mbappe ndiyo kipaumbele kikubwa pia wanatarajia kuwaleta wachezaji wengine kama Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund na Paul Pogba kutoka Manchester United.

Real Madrid iliwapa mikataba mipya wachezaji wao ambao watapata nafasi kubwa katika kikosi cha kwanza wachezaji hao saba ni Lucas Vazquez(2024) Nacho(2023) Dani Carvajal(2025) Thibaut Courtois(2026) Karim Benzema (2023) Federi Valverde(2027) na mchezaji mwingine ni Luka Modric ambaye amesaini mpaka 2022 anapaswa kulinda kiwango chake ili aweze kuendelea na mwaka bila matatizo.

Marcelo, Isco na Gareth Bale hawana uhakika na hatima zao kwani mikataba yao inaacha kufanya kazi mwaka 2022 na huenda wakaondoka klabu hapo.


USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

INGIA MCHEZONI HAPA

Acha ujumbe