Baada ya Mreno, Jose Mourinho kufungashiwa virago vyake kuwanoa mashetani wekundu, bodi ya matajiri hao imekaa na kutathmini juu ya nani ainisuru timu yao katika muda uliobakia kwenye msimu huu. Mkongwe na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Ole Gunner amekabidhiwa timu hiyo bila kinyongo akisaini kandarasi ya kuifundisha mpaka mwisho wa msimu 2018/19.
Anafahamika kwa jina la utani kama Baby-Faced Assassin tangu alipokuwa akiichezea United miaka ya 1996-2007, akijizolea umaarufu huo kutokana na uwezo wake aliokuwa nao katika umaliziaji wa mipira na kubadili matokeo wakati wowote wa hatari na kuinusuru timu akiwa uwanjani. United wanamkumbuka kwa makubwa aliyoyafanya mwaka 1999 pale Camp Nou [akiwa kama mchezaji] walipoumana na Bayern Munich kwenye fainali ya Klabu bingwa barani Ulaya[Champions League], alipoipatia United ushindi katika dakika za lala salama na kuifanya United kubeba kikombe kile.
Kwa sasa anarudi klabuni apo katika jukumu tofauti kabisa la kurudisha heshima heshima na hadhi ya klabu hiyo, baada ya kuwa na mwanzo mbaya kwenye ligi ikilinganishwa na miaka yao 28 ya nyuma waliyokuwepo kwenye ligi hii.
Awali, alikuwa akiifundisha timu yake iliyomlea kabla ya kusajiliwa na United pale Norway inayofahamika kwa jina la Molde akiwa kama kocha. Anakabidhiwa jukumu hilo kwa wakati huku matajiri wakiwa katika mawindo ya kumpata mrithi wa kudumu kwa misimu inayofuata. Katika historia yake ya soka pale United ameweza kushinda makombe sita[6] ya ligi, mawili ya shirikisho [FA] na klabu bingwa Ulaya.
Vile vile aliwahi kuiongoza Cardiff katika mzunguko wa pili wa ligi ya Uingereza msimu wa 2013/14 ili ainusuru timu kushuka daraja, na hakufanikiwa kuinusuru timu hiyo. Msimu wake akiwa kama mchezaji uliishia 2007 baada ya kupata majeraha makubwa ya mguu na kushindwa kurejea uwanjani, ndipo akaamua kuachana na soka la kucheza. Ameifungia United jumla ya mabao 126 katika mechi zake zote 366 alizocheza klabuni hapo.
Kwa wakati ulipo, nafasi yake na hali waliyonayo United ataweza kuleta umoja na muunganiko katika timu aliyoikuta na kujenga ari mpya ya kuipenda timu yao kutokana na mapenzi aliyonayo katika klabu hiyo iliyothamini uwezo wake.


Furahav
Ole ni kocha mzuri sana.