Historia: Hakuwa Kwenye Mipango ya Munich

Baada ya kuwepo kwa fununu za muda mrefu juu ya kocha wa zamani aliyeweza kufanya makubwa na klabu ya Arsenal kwa wakati ule, Arsene Wenger kuanza kuhUsishwa na kujiunga na klabu ya Bayern ambayo hadi sasa haina kocha mkuu kwenye safu ya uongozi wake wa kiufundishaji.

Yaliibuka mengi kwamba huenda mtu sahihi kuweza kupewa nafasi hiyo alikuwa ni Mzee Wenger ambaye ameweza kuonekana kama yupo karibu sana na klabu hiyo na hata aina ya soka ambalo linachezwa na klabu hiyo halima utofauti kabisa na lile ambalo Wenger alikiwa akilifundisha alipokuwa na Arsenal.

Masuala ya kimfumo kwa hakika yasingeweza kumpa shida yoyote Wenger kwa sababu kile alichokifanya akiwa mkufunzi alikuwa anakirejesha katika klabu hiyo. Uchezaji wa padi nyingi na kasi ya kudhambulia ulikuwa ni aina ya mfumo wa Wenger japo kwake hakuwa na madhambulizi ya kulazimisha kama yale ya City, huenda kutokana na viungo aliokuwa nao.

Lakini taarifa za kwamba kocha huyo angeweza kuifunza klabu hiyo zimeweza kuondoshwa kwa sasa na hazipo kabisa kinachoangaliwa ni kuendelea kwanza na kocha aliyepokea mikoba kutoka kwa Kovac ambaye aliweza kuondoshwa mapema mwezi huu na uongozi wa klabu hiyo kutokana na mwenendo wa matokeo wa klabu hiyo.

Wenger aliweza kujichomoa kabisa kwa kusema hakuwahi kukaa chini na uongozi wa klabu hiyo wakajadili juu ya yeye kuifundisha klabu hiyo. Kwanza hajafikiria kabisa kuwa Meneja wa klabu hiyo kwa wakati uliopo. Na kwa siku za usoni hatazamii kabisa kuwa sehemu ya uongozi klabuni hapo anachokiangalia kwa sasa ni kuendelea na mapumziko yake ya ukufunzi akiamini ni wakati ambao yupo huru zaidi.

Hans Flick ndiye aliyekaimu nafasi ya Kovac ndani ya klabu hiyo na huenda akiendelea na matokeo ambayo ameyaanza dhidi ya klabu hiyo mwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya ikaweza kumpeleka mbele zaidi na kuchukua nafasi hiyo. Japo Bayern ni klabu kubwa ambayo inahitaji kocha mwenye jina ili kuweza kuijenga zaidi. Uwepo wa makocha wakongwe huwa na chachu ya kuchochea ubingwa ndani ya klabu husika kwa sabahu ni masuala ya kirekodi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.