Orodha ya wachezaji wanaogombania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tisa katika ligi kuu ya Uingereza yatoka rasmi leo.

Ni utaratibu ambao upo kwa miaka mingi kwenye ligi hiyo yenye mvuto zaidi duniani kila mwezi inatolewa tuzo kwa mchezaji aliefanya vizuri zaidi kwa mwezi huo.

orodhaOrodha hiyo imejumuisha wachezaji sita kutoka vilabu sita tofauti mchezaji Kevin de Bruyne kutoka klabu ya Manchester City yupo kwenye orodha hiyo,Marcus Rashford kutoka Manchester United, Joseph Billing kutoka Afc Bournamouth, Alex Iwobi kutoka klabu ya Everton, Pierre emile Holjberg kutoka Spurs, pamoja na Jacob Ramsey kutoka klabu ya Aston Villa.

Wachezaji hao waliopo kwenye orodha hiyo, ndio watagombania tuzo baada ya kufanya kwao vizuri ndani ya mwezi wa tisa katika ligi kuu ya Uingereza na vilabu vyao ndio imefanya kuwepo kwenye orodha hiyo atakaefanikiwa kupata kura nyingi na kukidhi vigezo basi ataibuka mshindi wa tuzo hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa