Mchezaji nyota wa klabu ya Manchester United Paul Pogba amesema bado hajafanya maamuzi yoyote ikiwa atabaki au ataondoka huku mkataba wake ukitarajiwa kuisha mwezi June na kuwa mchezaji huru.
Paul Pogba, ambaye kwa sasa anamiaka 29 amekuwa mchezaji kijana kufikisha michezo 90 ambayo ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa siku ya ijumaa, wakati anahojiwa alisema, “sijafanya maamuzi yoyote mpaka sasa, hakuna kilichofanyika. Naweza kuamua kesho, naweza kuamua siku ya dirisha la usajiri tu, nataka kumaliza msimu vizuri.
“Huu msimu bado haujaisha bado, lakini hatupo kwenye nafasi ya yeyote ya kuweza kushinda taji lolote, nahitaji kushinda mataji, kucheza kwa ajiri ya kitu fulani lakini kwa mwaka huu na miaka michache iliyopita hatujafanikiwa kushinda taji lolote, inakatisha moyo.
“Kucheza kwenye timu ya taifa kunanipa amani, huo ndio ukweli. kulikuwa na kipindi kigumu kwa kipindi fulani pale United na nilihitaji haya mapumziko ili kuweza kupata hii nguvu na hali ya kujiamini.
“Kuna muda nilikuwa sichezi au matokeo mabovu, kuja hapa, inaniamsha morale, kuweza kupumzika na kupumua kunanisaidia mimi kurudi vizuri kwenye klabu.”
Paul Pogba ni miongoni mwa wachezaji watano ambao mikataba yao inaisha kwenye klabu ya manchester United wakiwemo, Jesse Lingard, Juan Mata na Edinson Cavani ambao wanatarajia kusaini kwenye klabu zingine huku golikipa Lee Grant akiwa kwenye mpango wa kupewa mkataba mpya wa kuwa mkufunzi.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.