Mchezaji Timo Werner amedai anafurahia kucheza katika mfumo wa timu ya taifa kuliko ule wa klabu yake ya Chelsea baada ya mshambuliaji huyo kufunga goli katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Israel mchezo wa kirafiki wa kimataifa siku ya Jumapili.
Goli la Werner lilikuwa ni goli la 22 katika michezo 48 aliyoicheza timu ya taifa ya Ujerumani lakini ameshindwa kufanya vyema katika klabu ya Chelsea akifanikiwa kufunga mabao 7 kwenye michezo ya 28 msimu huu na amedai Flick anamtumia kwa usahihi kuliko Tuchel.
“Mimi ni mshambuliaji na wakati wote nataka kufunga,” alisema Werner
“Vitu hajaenda kama nilivyokuwa ninataka pale Chelsea kwa hiyo ni bora vitu hivyo vinaenda poa chini ya Hansi Flick.
“Nafurahia mpira wa miguu haijalishi nipo wapi tofauti ni mfumo wa uchezaji wa Chelsea na hapa.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.