Real Madrid Kuwatema Wachezaji Sita

Klabu ya Real Madrid imepanga kupunguza mzigo wa wachezaji ili kupisha nafasi ya wachezaji wapya ambao klabu inapanga kuwasijiri kwenye majira ya kiangazi huku Eden Hazard na Marco Asensio yakiwa majina makubwa ambayo yanatarajia kuonyeshewa njia.

Real Madrid wamepanga kufanya matumizi makubwa kwenye dirisha la usajiri wa majira ya kiangazi, baada ya raisi wa klabu hiyo Florentino Perez kutaka kufanya usajiri wa majina makubwa wakiwemo Mbappe na Haaland kama usajiri wao wa kwanza muhimu.

Wachezaji amabao siku zao za kubakia kwenye kikosi cha Los Blancos zinahesabika, ni Eden Hazard ambaye amekuwa akisumbuliwa na mejeruhi ya mara kwa mara tokea asajiriwe na klabu hiyo, Marco Asensio  nae ataonyeshewa mlango wa kutoka.

Ukiachana na majina hayo makubwa kwenye kikosi cha Real Madrid, wengine ni washambuliaji wa kati Luka Jovic na Mariano Diaz nao wapo kwenye list ya kuondolewa, pia kiungo Dani Ceballos, ambaye anahitajika na klabu yake ya zamani ya Real Betis na mlinzi Jesus Vallejo nae ataoneshewa njia ya kutoka.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

 

 

Acha ujumbe