Manchester City kama zilivyobaadhi ya timu zingine kubwa, zimeuanza msimu wa 2020/21 kwa kusuasua. Licha ya kuonesha kiwango cha kupanda na kushuka, Pep Guardiola anasisitiza mvua ya magoli itakujua.

City wamekuwa wakishambulia timu nyingi lakini wanaupungufu mkubwa wa magoli ya kufunga kuliko ilivyozoeleka kwa timu hiyo.

Mchezo dhidi ya Olympiakos kwenye Ligi ya Mabingwa ni kielelezo sahihi katika hili. Pep Guardiola alishuhudia timu yake ikiutawala mchezo huo kuanzia mwanzo, City walipiga jumla ya mashuti 22 yaliyolenga goli la wapinzani ila waliambulia goli 1 tu.

Ilkay Gundogan na Bernado Silva walikosa nafasi za kupachika magoli katika ushindi uliowahikikishia City hatua ya 16 bora kwenye Mashindano ya Ligi ya Mabingwa.

Baada ya ushindi huo uliopatikana dakika ya 34 kwa goli pekee lililofungwa na Phil Foden aliyeitumia pasi nzuri kutoka na Rahim Sterling, Guardiola alisema ” (Magoli) yatakuja. tunapenda kufanya kazi zaidi, lakini siku moja yatakuja na tutavunja kila kinachosemwa.

“Tulicheza vizuri kwenye kila idara. Tumeshafuzu kwenye hatua inayofuata, sasa tunaweza kuitazama zaidi Premier League na mashindano mengine.”

Manchester City watawakaribisha Burnley kwenye dimba la Etihad wikiendi hii katika muendelezo wa michezo ya EPL.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

18 MAONI

  1. Pep Guardiola alishuhudia timu yake ikiutawala mchezo huo kuanzia mwanzo, City walipiga jumla ya mashuti 22 yaliyolenga goli la wapinzani ila waliambulia goli 1 tu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa