Tangu kuanza kwa msimu huu, Jurgen Klopp ni miongoni mwa makocha wanoitupia lawama EPL kwa upangaji wa ratiba hasa kwa timu zinazocheza mashindano mengi.

Turudi nyuma kidogo, Manchester United walitoka kucheza nchini Uturuki (Jumatano) na timu ya Istanbul Basaksehir ambapo walipoteza kwa kufungwa 2-1 na walitakiwa kucheza na Everton siku ya Jumamosi mchana.

Kitu hicho hicho kinatokea kwa Liverpool wiki hii, baada ya kucheza jana kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atalanta, watasafiri kuwafata Brighton Albion jumamosi mchana. Ni siku 2 tu za kupumzika na kujiandaa na mchezo huu.

Upangaji huu wa ratiba ni kati ya vitu ambavyo Jurgen Klopp anavilaani kwani vinawaumiza wachezaji kwa kiasi kikubwa.

Jurgen Klopp ameiambia BT Sports kuwa ” ninaogopa kusema lakini ninadhani haitotokea kwetu tu bali na kwa timu zingine pia.

“Unatupanga sisi kucheza Jumamosi saa 9:30 mchana, huo ni uhalifu kusema ukweli. Hiyo haihusiani chochote na mchezo wetu wa leo usiku (dhidi ya Atalanta).

“Ninachoshukuru kwa sasa ni kwamba sijapata majeruhi wengine. Kwa sasa tunatakiwa kuwa fit haraka sana. Wachezaji hawajafurahia matokeo lakini hatuna muda na hilo kwa kweli.

“Ni suala la kujiandaa upya na kuendelea mbele.”

Kipigo cha Liverpool kinawafanya waendelee na mchakato wa kuisaka nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa, wanahitaji ushindi katika mechi 1 tu kati ya 2 walizobakiwa nazo ili wafuzu kwenye hatua hiyo.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa