Raisi wa klabu ya Novara ambayo inashiriki ligi ya Serie C Italia Marcello Cianci ameamua kujiuzulu wadhifa wake kama meneja wa klabu hiyo baada ya kupatikana na bahasha yenye kiasi cha pesa cha €200,000 ambacho alicshindwa kukielezea chanzo chake.
Marcello Cianci amekuwa raisi wa klabu hiyo tangia mwaka 2019 na alikuwa anaendelea vyema na majukumu yake kabla hajaamua kuwajibika kufuatia kisa hicho.

Kwa mujibu wa chapisho la La Gazzetta dello Sport, bwana huyo mwenye miaka 50 alisimamishwa na askari katika eneo la Reggio Calabria, askari hao walimuona akiwa na bahasha yenye pesa €200,000, bahasha ambayo inaripotiwa kuwa ilifichwa kwenye boksi lililokuwa na chakula.
Raisi huyu anayestaafu alishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha juu ya uwepo wa pesa na kiasi hicho cha pesa kikazuiliwa na polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Tamko la klabu ya Novara Calcio limebainisha kuwa sakata hilo halina uhusiano kwa namna yeyote na klabu na ni swala binafsi kabisa linalomuhusu Cianci.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Sania
Kwa style hii rushwa haiwezi kuisha duniani
Adelta
Rais anatakiwa achunguzwe kwa kina
Magdalena
Uchunguzi ufanyike ili kila kitu kikae sawa
Khadija
kumbe rushwa hipo kila sehemu
Neema juma
Rushwa sio poa hata kidogo
Caroline
Hii skendo imemchafua sana
Dorophina
Kwa stahili hii anaichafulia klabu yake jina
Rahma
Rushwa sio kitu kizuri
Hopemwaikuka
Janga la dunia yote
Venerose
Rushwa noma
Lydia Emmanuel Magoti
Duuh Sio poa
Issa
Sio poa
warda
Jamani si angeiweka vizuri tu