Imeripotiwa kuwa, klabu ya AFC Leopards inayocheza ligi kuu nchini Kenya. Ipo katika mazungumzo ya kumkabidhi timu Patrick Aussems.
Leopards wamekuwa bila kocha mkuu baada ya Tomas Trucha kuacha kazi kwa kile alichodai kuwa baadhi ya maofisa wa klabu hiyo walikuwa wakimuingilia kwenye majukumu yake.
Tangu kuondoka kwa Trucha, Leopards imekuwa chini ya kocha msaidizi – Anthony ‘Modo’ Kimani na sasa uongozi wa klabu hiyo umepanga kumpatia kibarua cha ukocha mkuu, Patrick Aussems ambaye aliondolewa kwenye nafasi yake Simba SC – Tanzania.

Tangu alipoondolewa Simba, Patrick amekuwa nje ya uwanja na sasa chanzo cha kuaminika, kimethibitisha kuwepo kwa mazungumzo kati ya kocha huyo na klabu ya AFC Leopards.
“Tumekuwa na mazungumzo na Aussems na sasa tupo kwenye hatua nzuri zaidi. Kama tukikubaliana kwenye vitu vichache, basi Jumamosi atatangazwa kama kocha wetu.
“Ni kocha mzuri ambaye atatusaidia kuyafikia malengo yetu kutokana na uzoefu wake kwenye kazi hii. Kama Ingwe, tunajiamini tunaweza kupambania makombe makubwa, kwa sababu hiyo, tumeamua kumchagua mtu sahihi.” alisema kiongozi mkubwa wa AFC Leopards.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Sania
Habari njema kwetu mashabiki
Adelta
Hili ni bonge la makala nzuri yenye maelezo mazuri
Magdalena
Kwa mashabiki imekaa poa sana
Sarah
Habari nzuri kwa mashabiki
Khadija
kwa upande wa mashabiki imekaa poa
Neema juma
Hii iko poa sana
Dorophina
Nice update
Caroline
Asante kwa taarifa
Rahma
Asante meridinia kwa makala
Hopemwaikuka
Imeeleweka
Venerose
Makala iko pouwa
Lydia Emmanuel Magoti
Hiko poa hii
Issa
Kaz njema
warda
Aussems anapenda sana Africa