Raphael Varane amerejea kujiunga na kikosi cha kwanza cha Manchester United katika maandalizi ya safari ya pambano dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye wiki ya 10 ya gemu za Ligi Kuu Uingereza.

Beki huyu alishindwa kucheza mechi tatu zilizopita baada ya kupata jeraha alipokuwa kwenye majukumu ya kitaifa mapema mwezi huu.

Staa huyu alitarajiwa labda angerejea uwanjani hapo Novemba, lakini ameonekana uwanjani katika mazoezi na kikosi cha kwanza mapema kuelekea mechi ya jumamosi.

Raphael Varane Arejea Kuelekea Kuvaana na Spurs

Staa huyu, amecheza jumla ya mechi saba za Man United tangia alipowasili klabuni hapo toka Real Madrid msimu wa joto, mechi tano zikiwa za Ligi Kuu.

Mashetani wekundu wamekuwa na kipindi kigumu kwa wakati Varane alipokuwa nje ya dimba, wakiruhusu magoli 11 kwenye mechi za michuano yote dhidi ya Leicester City, Atalanta BC na Liverpool.

Bila shaka, meneja wa Man United, Ole Gunnar ataizungumzia hali ya mchezaji huyu kwenye mkutano na waandishi wa habari Ijumaa, na kubainisha nafasi yake katika mchezo Ujao.


MCHONGO WA PESA NA CIRCUS FEVER

Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa