Rasmi Roberto Martinez Asaini Mkataba Mpya

Shirikisho la soka la Belgium (KBVB) limetangaza kuwa Roberto Martinez amesaini mkataba kusalia Belgium kama kocha mkuu hadi 2022.

Martinez aliteuliwa na Belgium mwaka 2016, mkataba wake mpya unampa nafasi ya kuendelea kusalia klabuni hapo hadi mwaka wa Kombe la Dunia la Quatar 2022.

Kocha huyu Mhispania aliwaongoza kikosi cha Belgium maarufu kama “Golden Generation”, huku uswahilini tunaweza kusema “Kizazi cha Dhahabu” hadi kufikia nusu fainali za Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 ambako Ufaransa waliamua kuwabania riziki kwa kuwapa kichapo kabla ya kuwalaza Uingereza na kuchukua ubingwa wa dunia.

Rasmi Roberto Martinez Asaini Mkataba Mpya
Roberto Martinez Aliwaongoza Belgium hadi Nusu Fainali Kombe la Dunia Urusi

Mkataba wake wa sasa ulikuwa unaisha baada ya michuani ya Euro 2020 ambayo imesogezwa mbele kwa mwaka mmoja zaidi kwa sababu ya janga la corona.

Belgium ambao kwa sasa wapo kwenye kilele cha FIFA kwa timu bora zaidi, walikuwa moja ya timu zilizotarajiwa kuondoka na ubingwa wa dunia baada ya kufanya vyema katika hatua za awali toka kufuzu mpaka walipoingia nusu fainali.

Tangazo la Belgium limenogeshwa na Hazard!

Tangazo limeambatana na video fupi ya kapten wa Belgium na nyota wa Real Madrid, Eden Hazard akicheza gemu ya video maarufu ya FIFA huku akivunga kama anapokea simu ya nchezaji mwenzake Romelu Lukaku.

Kwenye video fupi Hazard anasema:

“Kocha amesaini! Kocha amesaini, ole ole ole. Mambo Romelu, umeona kocha kasaini? ndiyoo si ni taarifa njema hizi! Haya kwaheri”

Belgium na Martinez wanatarajia kuongea na vyombo vya habari Jumatano hii ili kuzungumzia suaola la mkataba wake mpya.

45 Komentara

    Coach Bora Robert Martinez..amestahili kuongezewa mkataba.#meridianbettz

    Jibu

    ahsante meridian kwa taarifa#meridianbettz

    Jibu

    Duuu asante kwa kutujuza #meridianbet

    Jibu

    Martinez anafanya vizuri sana kwenye machaguzi yake ya wachezaji na ndio maana Belgium wanafanya vizuri sana

    Jibu

    inapendeza na ni hatua nzuri

    Jibu

    Good news to Belgium team #meridianbettz

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Hongera Martinez @robArt (kibala) kwa kuongezwa mkataba kila la kheri na mafanikio tele kwny majukumu yako ya kazi thanks meridian kwa habar za michezo na burudani

    Jibu

    Safi sana Martinez ni bonge la kocha anastahili kuendelea kuinoa Belgium

    Jibu

    Coach mzuri sana..!nategema mabadiliko kutoka kwako

    Jibu

    Ni kocha nzuri Sana akiwa kwenye kazi yake

    Jibu

    Inapendeza sana kwa hatua aliyo ifikia ya kuwa kocha mkuu

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Ni kocha anaejituma sana anastahili kuongezwa mkataba

    Jibu

    Anastahili pongezi kwa kazi nzuri.

    Jibu

    Ni kocha mzuri sana ambaye anajua kujituma safi sana

    Jibu

    Habari nzr asanteni kwa kutujulisha

    Jibu

    Anastahili

    Jibu

    Mambo mazuri hayo

    Jibu

    He deserve it #meridianbettz

    Jibu

    Inapendeza sana

    Jibu

    Ni Kocha mzuri na amepata mafanikio kiasi fulani lakini anahitajika kufanya zaidi ili kizazi cha dhahabu kilete vikombe #Meridianbettz

    Jibu

    Yuko vizuri hana masihala kwenye kazi yake,,namkubali kinoma💪

    Jibu

    Yupo vizuri.

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Ahsanteni kwa kutuhabarisha meridianbet

    Jibu

    Habar njema # meridianbet

    Jibu

    Hongera zake

    Jibu

    AMeisaidia timu kwa kiasi kikubwa, vizuri aendelee kuitumikia Belgium kwa awamu nyingine tena

    Jibu

    Habari njema kabisa kwa sisi tunaomuelewa Martinez.
    #meridianbet

    Jibu

    Ni habari nzuri sana kwa wapenzi wa soka wa nchini kwao

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Hongera kwakeee kwa kujituma vyema

    Jibu

    Safi sana kocha kwa kuongeza mkataba mwingine

    Jibu

    Hongera kicha bora.

    Jibu

    Ni habari nzuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

    gud newz asante

    Jibu

    Namkubali Sana Mana ni kocha anayejitambua na asiyekurupuka katika kufanya chaguzi za wachezaji

    Jibu

    anastahili pongezi kwake

    Jibu

    Nikocha mzuri Sana hana stairi pongezi

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Asante meridiani kwa taarifa njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.