Ndoto ya Eden Hazard kuhamia Real Madrid aliyokuwa nayo kwa muda mrefu, imegeuka kuwa jinamizi linaloziwinda pande zote mbili, huku kumaliza mkataba kwa mapema zaidi kukionekana kuwa suluhisho pekee.

Baada ya kutumia pesa nyingi kumnunua winga huyo kutoka Chelsea, Real Madrid wamekuwa wakisita kumuuza, na sasa ikiwa imesalia miaka miwili tu kwenye mkataba wake jambo hilo linaibuka, huu ni wakati wa kufanya makubaliano.

Kwa mujibu wa Foot Mercato, Arsenal wanahitaji huduma ya staa huyu, na tayari wamewasiliana na winga huyo wa Ubelgiji kuhusu uwezekano wa uhamishio msimu huu wa joto.

Mpango ni kumpata Hazard kwa mkopo, kukiwa na matumaini kuwa anaweza kucheza mara kwa mara kwa mwaka mmoja, kisha kumuuza majira ya joto yajayo kwa ada ya kawaida, wakati mwaka mmoja ukiwa umesalia kwenye mkataba wake.

Bila shaka hii ni sandakalawe kwa Arsenal kama ilivyo kwa Real Madrid. Nyota huyo wa zamani wa Chelsea anaweza kutumia mwaka mwingine kuitafuta thamani yake inayoonekana kuporomoka zaidi akiwa La Liga. Lakini kutokana na kwamba hachezi kwa sasa, ni kama kamari ambayo pengine inafaa kuchukuliwa kwa pande zote.

Real Madrid Wawasiliana na Arsenal Juu ya Hazard


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa