Breaking News: Ronaldo Akubali Kusaini Mkataba na Al Nassr ya Saudia

Imeripotiwa kuwa Cristiano Ronaldo amekubali kusaini mkataba wa paundi milioni 172.9 kwa mwaka na klabu ya Al Nassr ya nchini Saudi Arabia.

 

ronaldo

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alikatishwa mkataba wake wa Manchester United mapema mwezi huu, kufuatia uhusiano wa kutatanisha na wakuu wa klabu ambao ulizidi kuwa mbaya zaidi alipotoa kauli nyingi za kutatanisha katika mahojiano ya televisheni na Piers Morgan.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alikuwa akishinikiza kuondoka Old Trafford majira ya joto, lakini hakupata matakwa yake kwani alidhamiria kucheza soka la Ligi ya Mabingwa (UCL).

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid alikataa kuhamia Saudia majira ya joto yaliyopita, lakini bila maslahi yoyote kutoka kwa vilabu vya Ulaya, anaonekana kuwa tayari kuhama.

 

ronaldo

Inasemekana Ronaldo amekubali mkataba wa miaka miwili na nusu na Al Nassr wenye thamani ya paundi milioni 172.9 kwa mwaka ambao utamfanya acheze hadi umri wa miaka 40, kwa mujibu wa jarida la Hispania la Marca.

Al-Nassr ni moja ya vilabu vilivyofanikiwa zaidi nchini Saudi Arabia, ikiwa imetawazwa washindi wa ligi kuu ya nchi hiyo mara tisa, na ushindi wao wa hivi karibuni ulikuwa ni wa mwaka 2019.

Ripoti hiyo hiyo pia imependekeza kwamba hakuna klabu kutoka Ulaya au ya Marekani (MLS) inaweza kumudu kutoa kiasi kilicho karibu na ofa hiyo ya kifahari.

Chelsea pia wamepunguza hamu yao ya kumnunua Ronaldo huku miamba wa Bundesliga Bayern Munich wakikataa mazungumzo mapema wiki hii tangu mahojiano yake ya bomu ambapo alimkashifu mmiliki na meneja wa United Erik ten Hag.

Ronaldo, hata hivyo, bado yuko makini kwa wakati huu kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar huku akitafuta kusaidia Ureno kuongoza kundi lao watakapomenyana na Korea Kusini Ijumaa alasiri.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

CHEZA HAPA

 

ronaldo

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.