Ronaldo Kuendelea Kuvaa Uzi wa United Msimu Ujao?

Mashambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo leo amejumuishwa kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu kutoka nchini Hispania Rayo Vallecano kwenye dimba la Old Trafford.

Baada ya sintofahamu kuhusu hatma ya mchezji huyo wa kimataifa kutoka nchini Ureno kwenye viunga vya Old Traford hatimaye leo kavaa jersey na kufanikiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kutoka na nafasi kuchukuliwa na Amad Diallo.

 

Ronaldo hakusafiri na timu kwa ajiri ya michezo ya kujianda na msimu huu kutokana na sababu za kifamilia ambazo klabu ilitoa taarifa na na kupelekea kukosa mchezo didi ya Liverpool nchini Thailanda na ule wa atlatico madrid jijini Oslo.

Ronaldo atakuwepo kwenye kikosi. Na tutaangalia ni muda gani anaweza kucheza,” Kabla ya mechi Ten Hag aliuwambia mtandao wa klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amebakisha mwaka mmoja kwenye kandarasi yake, na yuko tayari kusamee kitika cha mshahara wake ili aweze kuhama klabu hiyo.

Man Utd msimu uliyoisha ilifanikiwa kumaliza nafasi ya sita kwenye ligi kuu nchini Uingereza, na kupelekea kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani, sasa wanatarajia kwenda Kushiriki michuani ya Europa League msimu huu na wataanzia mzunguko wa pili.

Je Ten Hag atafanikiwa kumshawishi Ronaldo aendelee kubaki kwa msimu mmoja zaidi?


 

Acha ujumbe