Sancho Amuenzi Floyd kwa ‘Hat-Trick'

Nyota wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza, Jadon Sancho ameonesha hisia zake juu ya kifo cha mmarekani mweusi, George Floyd alieuawa na polisi nchini Marekani kwa kuonesha fulana iliyoandikwa ‘Justice for Floyd’ aliyovalia ndani ya jezi katika mchezo wao wakiwawabili Paderborn.

Hatua hiyo imetafsiriwa kama kuwaunga mkono mamia ya waandamaji katika miji mbalimbali nchini Marekani wanaoandamana ili kushinikiza haki itendeke juu ya tukio hilo lililotokea katika mji wa Minneapolis.

Nyota huyo wa kimataifa wa England, alionesha fulana hiyo bada ya kufunga katika yenye maandishi “Justice for George Floyd” baada ya kufunga goli moja katika ushindi wa magoli 6-1 waliyoshinda huku yeye pekee akifunga matatu katika hayo.

Magoli mengine ya Dortmund yalifungwa na Marcel Schmelzer na Achraf Hakimi ambaye nae alionesha fulana yenye maandishi sawa na ile ya Jadon Sancho, ‘Justice for George Floyd’. Hata hivyo tukio hilo lilipelekea muamuzi wa mchezo huo amzawadoe Sancho kadi ya njano!

Magoli hayo matatu ya Sancho yanamfanya Sancho kuwa amehusika katika magoli 33 (yote ya kufunga na assists) na kuwa mchezaji aliyehusika katika magoli mengi zaidi katika ligi zote kubwa Ulaya nyuma ya Robert Lewandowski.

Ushindi huo wa kishindo wa Borussia Dortmund ni majibu kwa kipigo cha goli moja kwa bila walichokubali kupokea kutoka kwa mabingwa Bayern Munich na unafanya wazidi kujikita katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ‘Bundesliga’ wakiwa na alama zao 60 nyuma ya vinara Bayern Munich wenye jumla ya alama 67 kileleni katika msimamo.

42 Komentara

    Kafanya jambo jema sana

    Jibu

    Pole sana ila naamini haki itatendeka

    Jibu

    RIp George floyd

    Jibu

    Safi sana Sancho kwa kuiga mazuri ya George Floyd bila kificho na kuzidi kufanya vizuri uwanjani.

    Jibu

    Uwo ni ubinadam unaohitajika

    Kwakila binadam Sancho yupo sahii kumuenzi
    Pumzika kwa amani Floyd,

    Jibu

    Ubaguz ni tatizo sana kwa nchi za wenzetu hasa wachezaji weus wanabaguliwa sana

    Jibu

    Jadon amefanya jambo la maana.na lakiungwana.hakika Geogre hatosahaulika..r.i.p geogre

    Jibu

    Rip Floyd

    Jibu

    Justice for Floyd

    Jibu

    Tukio la mauaji ya mtu mweusi limesikitisha wengi mno kwa alichokifanya Sancho salute kwake

    Jibu

    Polen Sana dah ubaguz watu weusi ng’ambo cjui hutaish ln thnks meridian bet tz

    Jibu

    Daaa kifo chake kimewaumiza wengi sana

    Jibu

    Mbele yake nyuma yetu

    Jibu

    jambo la maana.na lakiungwana.hakika Geogre hatosahaulika..r.i.p geogre

    Jibu

    Geogre hatosaulika R.I.P

    Jibu

    Tunaomba haki itendeke

    Jibu

    R.I.P george floyd#meridianbettz

    Jibu

    Sancho ana moyo wa huruma ameonyesha kuguswa kwak

    Jibu

    Tutakukumbuka daima George

    Jibu

    Rip George

    Jibu

    Sancho solute # meridianbettz

    Jibu

    Amefanya vizuri sanaa maana Hawa jamaa weupe wanatufanya sisis Kama hatina haki ya kuishi

    Jibu

    Kafanya jambo zuli sana#meridianbettz

    Jibu

    Kafanya jambo jema sana

    Jibu

    kuna binadam wana roho mbaya yani kuonyesha furana tu wana muuwa

    Jibu

    Amenikumbusha maneno ya Mario Balloteli’ why always me’ ! Ameonyesha hisia zake lkn kwenye mchezo wa soka hairuhusiwi#meridianbettz

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Da kifo cha George kimemuuma kila mtu asiependa ubaguzi

    Jibu

    Ushindi huo wa kishindo wa Borussia Dortmund ni majibu kwa kipigo cha goli moja kwa bila walichokubali kupokea kutoka kwa mabingwa Bayern Munich

    Jibu

    Ichi kifo kimeniuma jmn.Mungu atawalipa

    Jibu

    Jamani inasikitisha sanasa

    Jibu

    we are appreciate for what he done to our beloved Floyd

    Jibu

    kama binadamu lazima uwe na hisia za kibinadam, alicho kifanya sancho ni jambo la kheli kwa kuonesha kwamba hajasapoti kilicho mkuta floyd

    Jibu

    Sancho fundi wa Mpira..siku chache zijazo huyooo man utd #meridianbettz

    Jibu

    Sancho ametukumbusha machungu ya mpendwa wetu thnks meridian bet tz

    Jibu

    Dah hatuwezi msahau George

    Jibu

    Hakika kwa wenzetu weupe bado hawajakaa kufikiria kuwa ata sisi watu weusi tunahaki ya kuishi na haki nyingine pia, ifike wakati watambue ata sisi ni kama wao, lucky Dube aliona mbali sana.

    Jibu

    Sancho ni noma kafanya vizuri kumuenzi

    Jibu

    Ameonyesha jinsi gani asivyopenda ubaguzi wa rangi.hongera

    Jibu

    Dah inaumiza sana

    Jibu

    Rip flloyd

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.