Shutma za Rais PSG

Rais wa klabu ya matajiri wa jiji la Ufaransa, Nasser Al-Khelaifi yupo katika kashfa nzito ya kujihusisha na manbo ya matumizi ya fedha nyingi kutaka kununua mashindano ya riadha mwaka 2017 yaliyokuwa na jina la 2017 World Athletics Championships jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni za FIFA.

Rais huyo ameingia kwenye tuhuma hizo za kujihusisha na masuala ya rushwa kutaka mashindano hayo kupigiwa upatu na yafanyike kule Doha kwa kujaribu kuwaRubuni baadhi ya viongozi wakubwa waliokuwa wanasimamia mashindano hayo kwa kipindi kile. Sakata hilo limeanza kufanyiwa utafiti sasa.

Jaji Renaud Ruymbeke amemtuhumu mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa beIN Media Group, pia, tajiri mwenye uwekezaji ndani ya klabu ya PSG chini ya Qatar Sports Investment kwenye sakata la kutumia kiasi cha $3.5M ikiwa kama sehemu ya malipo katika sakata hilo.

Malipo hayo yalifanyika kwa Rais wa awali wa riadha (IAAF), Lamine Diack kuhusiana na uendeshaji wa mashindano mazima 2017 World Championship. Kwa ripoti za jaji huyo ni kwamba Diack kwa sasa ni vigumu kukana mashtaka yake kutokana na uhalisia wa fedha zote kuona kwamba zilikuwa zikiingia na kutoka kwenye akaunti zake.

Diack anaonekana kuwa mhanga wa matukio mengi makubwa ndani ya shirikisho hilo kwa kuchepusha uhalisia na kuwa uongo hasa pale ambapo waliweza kubadili eneo ambalo mashindano hayo ilibidi yafanyike lakini alitumia nguvu zake na pesa alizoweza kuahidiwa kubadili matokeo kutoka kwenye uhalisia kwenda kwenye uongo. Kura nyingi za washiriki zilipendekeza yafanyike London lakini yalipinduliwa kabisa.

Kashfa hizo sio njema kwa Al-Khelaifi ambaye ni kiongozi mkubwa ndani ya kamati ya UEFA ambapo ni mwakilishi mkubwa sana wa klabu za Ulaya ndani ya kamati hiyo. Mapema Jumatano wanategemea kuwa na mkutano kule Baku ambako fainali za UEFA Europa zitafanyika na wao wakiwa ni wasimamizi wakubwa.

Mbali na hilo pia kuna taarifa kwamba wanajihusisha na kutumia nafasi zao kununua haki za kurusha matangazo ya kombe la dunia yatakayofanyika huko Qatar 2026 hata yale ya 2030 na sakata hilo bado lipo chini ya uchunguzi mkubwa hadi pale litakapotolewa ufumbuzi wake.

2 Komentara

    Mmh noma

    Jibu

    Duh noma sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.