Kocha mkuu wa klabu ya Namungo, Hemmed Morocco amekiri kuwa wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Simba utakaopigwa kesho mkoani Lindi.

simba

Namungo na Simba wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wao wa kiporo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, ambapo mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa timu hizo mbili kukutana msimu huu.

Tangu kupanda kwao Ligi Kuu Bara, Namungo wamekuwa na wakati mgumu mbele ya Simba ambapo katika michezo yao mitatu waliyokutana mpaka sasa, Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo miwili huku mchezo mmoja ulioisalia ukimalizika kwa suluhu.

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Morocco amesema: “Tunashukuru baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina katika mchezo wetu uliopita wa Ligi Kuu Bara, tunakabiliwa na mchezo mgumu wa Jumamosi (kesho) dhidi ya Simba, ambao tunajua wazi kuwa ni miongoni mwa timu bora kwa sasa.

“Lakini licha ya kutambua kuwa tunakwenda kukutana na wapinzani wagumu bado tumejiandaa kupambana, ili kuweza kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na kuzidi kumaliza katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo wa Ligi.”


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa