Simba Vs Yanga na Ufalme wa Nyamagana

Inaaminika ni mechi bora zaidi kuwahi kutoke kwenye ardhi ya Tanzania na Afrika Mashariki, inaaminika Haitokuja kutokea Derby ya Kariakoo kama ile tena, ni pale juu ya Kichuguu Nyamagana historia iliandikwa.

simba
Nyamagana Stadium

Ilikuwa ni fainali ya Kombe la Taifa ngazi ya vilabu, wakati huo Simba akiingia kama bingwa mtetezi baada ya kubeba kombe hilo 1973 baada ya kuifunga klabu ya Kigoma huko na pia alimpiga Yanga hatua ya Nusu fainali.

Ni mwaka huo huo Yanga ilienda kambi nchini Brazil na walikutana na Mfalme wa soka la dunia Pele, wakafanya mazoezi kwenye udongo mtakatifu wa soka! Wakati huo Simba walienda barani Ulaya kwenye nchi ya Poland, ardhi yenye mastraika wa roho mbaya zaidi.

Itoshe kusema ilipotimu mishale ya jioni ya Oktoba 10,1974 tayari Uwanja umetapika Mashabiki, hakuna pa kukaa wala kutema mate! Wananchi wanahanikiza kulipa kisasi huku Simba wakichagiza kubeba tena ndoo back to back.

Mtanange ulianza kwa kasi sana, lakini mapema Saad Ally wa Simba aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Sabu alieweka kambani dakika ya 16 tu ya Mchezo na mpaka Halftime Mnyama 1 na Yanga bila.

Kipindi cha pili Yanga walikuja kwa kasi sana, ndugu wawili wenye vipaji vikubwa Kitwana Manara na Sunday Ramadhan Manara waliwapa tabu sana mabeki Wa Simba, Omari Chogo Chemba na wenzie.

Wakati Mnyama wakiamini tayari mechi imeisha, dakika ya 87 mpira mrefu wa beki Ally Yusuf wa Yanga unamponyoka Omari Chogo na kutua kwa Gibson Sembuli alieweka shuti kali na kumpita kipa wa Simba Othman Mambosasa, ngoma ni 1-1 na mtanange unaenda 120 kwa mara ya kwanza.

simba
Kikosi cha Simba

Sunday Manara kwenye jioni bora ya maisha yake na jezi ya Wananchi, Anapokea pass kutokea chini anapangua ukuta wa Simba kisha anafungua inagongwa krosi kisha anazama nayo kwa kichwa, na kuipa Yanga bao la pili na wanabeba ndoo kwa 2-1, Wananchi wanamvua ubingwa Mnyama pale Mwanza.

Inakuwa mechi ya kwanza ya Watani kuchezwa nje ya Dar Es Salaam, mechi ya kwanza kwenda 120 na mechi ya kwanza watu wakiwa wametoka Camp nje ya bara la Afrika.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

9 Komentara

  Habari nzuri sanaa

  Jibu

  Derby haina viwango

  Jibu

  Hatari sana.

  Jibu

  Hatari sana

  Jibu

  Iyo sijaishuhudia

  Jibu

  Baraaa

  Jibu

  Inaonekana ilikuwa balaa Sana

  Jibu

  Noma sana

  Jibu

  Atar sanaa

  Jibu

Acha ujumbe