Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameweka wazi kwamba hatishiki na kiwango cha mahasimu wao kwa miaka ya hivi karibuni kwani wao bado ni bora.

Manchester City wameshinda mataji matano ya ligi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita wakati United akifanikiwa kuchukua mara moja katika kipindi hicho.
Pamoja na mafanikio yote, kuelekea mchezo wa leo Solskjaer anaamini timu yake bado ni timu bora katika jiji la Manchester, na itabaki hivyo kwa miaka mingi ijayo.!
“Hapana, Siwezi” Solskjaer alijibu alipoulizwa endapo anaweza kufikiria kama City inaweza kuwa kubwa kuliko United siku moja. “Lakini ipo hivi tunawaheshimu kwa kile walichofanya kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi, ukiongeza miaka minne au mitano waliofanya vizuri EPL na Ulaya.”
“Lakini sisi ni Man United, siku zote tunarudi katika nafasi yetu, Nadhani ni klabu bora Manchester na hiyo ikaanisha Duniani.”
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.


