Barcelona wamethibitisha leo kuwa tayari wamekamilisha dili la kumsainisha Xavi Hernández

kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, na bosi huyo mpya wa Barcelona anatarajia kuwasili wikiendi hii.

Staa huyu wa zamani wa klabu hiyo ya Barcelona, ametuma ujumbe wake kwa wapenzi wa timu ya Barcelona kuwa sasa “Anarejea nyumbani”.

Rasmi: Xavi Kocha Mkuu wa Barcelona Mpaka 2024

Xavi ametumia ukurasa wake wa Instagram kuchapisha ujumbe wake kwa mashabiki wa klabu hiyo.

“Ndugu wapenzi wa Barcelona, NAREJEA NYUMBANI”.

 

“Ninarejea mahali nilipokuwa, ninarejea kwenye klabu ya MAISHA yangu.

Sina maneno zaidi ya kuelezea jinsi ninavyojisikia kwa mara nyingine tena kuilinda ngao ambayo alama yake ipo moyoni mwangu, kuhisi kwa mara nyingine Camp Nou ikitetema, na kusikia tena sauti za furaha na kupeana moyo kutoka kwa mashabiki hawa bora.

 

Nina fahamu kuwa ninawasili katika kipindi kigumu, lakini ninaenda kupambana na changamoto hii kwa matumaini makubwa. Nitafanya kazi na kupigana kwa kushirikiana na ninyi wote kufikia mahali ambapo tunastahili kuwepo.

 

Nashukuru #Barcelona kwa kuniamini, na kwa mashabiki wote walioniamini kuwa ninaweza kuchukua jukumu hili muhimu.”

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Xavi Hernández (@xavi)


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa