Ni wakati wa Manchester Derby kunako EPL mchana huu, vita ya mbinu kati ya Ole Gunnar Solskjaer na Pep Guardiola. Nani ni nani?
United kuwaalika City ndani ya Old Trafford katika mchezo wa 11 wa EPL msimu huu, 2021/22. Huu ni miongoni mwa michezo mikubwa kwenye kalenda ya soka nchini Uingereza.
Kwa takwimu za hivi karibuni, United ameshinda michezo 3 kati ya 4 waliyokutana na City huku wakitoka sare mchezo 1. Ole amemzidi kete Pep katika hili. Japokuwa, msimu huu bado ni maseke kwa United.

Manchester United wanashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na alama 3 pungufu ya City katika nafasi ya 3, na alama 8 pungufu ya Chelsea ambaye ni kinara wa ligi mpaka sasa.
The Red Devils wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kupigwa 5-0 na Liverpool hapa hapa Old Trafford kabla ya kubadilisha mfumo na kuwafumua Spurs 3-0 na kutoa sare na Atalanta (2-2) kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kubadilika kwa mfumo wa Manchester United na kutumia 3-4-2-1, kutawasaidia kupata matokeo mchana huu? Au mfumo wa 4-3-3 wa Pep Guardiola utaongeza shubiri kwenye kibarua cha Ole Gunnar Solksjaer?
Dakika 90 ndani ya Old Trafford, TUNATOKAJE?
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.


