Bilionea na mmiliki wa mtandao wa kuperuzi miziki (Spotify), Daniel Ek anatarajiwa kutangaza dau lake la kuinunua klabu ya Arsenal.
Tangu kutokea kwa sakata la European Super League ambapo Arsenal walikuwa miongoni mwa vilabu 12 vilivyohusika kwenye mchakato wa ligi hiyo na baadae kujiondoa, kumekuwa na shinikizo miongoni mwa mashabiki wa vilabu vya EPL vilivyohusika kwenye mpango huo ambao umepingwa vikali barani ulaya.
Mmiliki wa Arsernal, Stan Kroenke kama ilivyo kwa familia ya Glazers wanaomiliki klabu ya Man United, anakumbana na shinikizo kali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo wakimtaka kuachana na klabu hiyo mapema iwezekanavyo.
Waswahili walisema, “Vita ya fisi, furaha kwa kunguru”. Mmiliki wa Spotify, Daniel Ek anadhani huu ni muda sahihi wa kuweka dau lake mezani na kuinunua timu ambayo amekuwa akiishabikia tangu utoto wake.
Mpango wa Spotify kuinunua Arsenal unatajwa kuwahusisha wachezaji watatu magwiji wa klabu hiyo. Thierry Henry, Dennis Bergkamp na Patrick Vieira wanaripotiwa kuwepo kwenye orodha ya Daniel EK kama watu atakaohitaji msaada wao katika mchakato wa kuinunua Arsenal.

Mpaka sasa, haijajulikana Daniel Ek ataweka dau la kiasi gani mezani kwa Kroenke ili awezekuuziwa klabu hiyo na pengine kuwa sehemu ya kumnusuru Kroenke dhidi ya hasira za mashabiki wa timu hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, siku ya Ijumaa Mmiliki wa Spotify [Daniel Ek] aliweka chapisho lililosomeka “wakati nakuwa kama mtoto, ninakumbuka nilikuwa nikiifurahia Arsenal. Kama KSE watataka kuiuza Arsenal, nitafurahi kuitupa kofia yangu kwenye ulingo (akimaanisha kutangaza dau la kuinunua)”
KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.
Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?



dorophina
Habari njema
Venerose
Asante kwa taarifa
Issa
Hata Europer Hawagus msimu huu
Mariam mtandama
Habar njema meridien
Johnmary jo
Habari njema hiyo#meridianbett
aisha
Habari njema
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
Adelta
Inapendeza
Sarah
Vizuri
Saupha mohamed
Nice
Magdalena
Good
Theonestina
Habari njema
Khadija
Habari njema