Huu ni mwezi wa Newcastle United kwenye ulimwengu wa habari duniani. Kuuzwa kwa klabu, hatma ya Steve Bruce kama kocha n.k. Bruce bado yupo yupo!
The Magpies bado hawajaonja ladha ya ushindi kwenye EPL mpaka sasa, matokeo ya kusuasua yamewagawa mashabiki wa klabu hiyo kwa muda mrefu. Takwa mojawapo la mashabiki lilikuwa ni mmiliki wa awali, Mike Ashley kuachia timu. Hili limefanikiwa.
Sasa Newcastle United ipo mikononi mwa wamiliki wapya ambao wanaumiliki wa 80% kwenye klabu hiyo. Japokuwa, umiliki huu umezua gumzo kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia, suala la kocha mpya limekuwa gumzo.

Steve Bruce aliweka wazi kile anachokiona kabla na baada ya Mike Ashley, kocha huyu alisema wazi kuwa hana uhakika wa kuendelea kusalia St James Park na hivyo ni suala la muda tu, ataachishwa kazi.
Mpaka sasa, hili halijatokea na sasa ni rasmi, Newcastle United wamethibitisha Steve Bruce ataiongoza timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Hot Spurs wikiendi hii. Huu utakuwa ni mchezo wa 1,000 kwa Bruce katika maisha yake ya ukocha.
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

