Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Aurelien Tchouameni anaonekana kuanza kurudisha ubora wake katika kikosi hicho cha mabingwa wa muda wote wa ulaya.

Tchouameni alionekana kupoteza ubora katika msimu uliomalizika baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia na kiungo huyo kupata majeraha jambo lililomfanya kupoteza nafasi ya kudumu katika kikosi cha Real Madrid.TchouameniKiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua kwenye kiwango bora saba katika michezo miwili ambayo klabu ya Real Madrid imecheza michezo hiyo ni dhidi ya Ac Milan na Man United ambapo kiungo huyo kaonesha ubora wa hali ya juu.

Kiungo Tchouameni kama ataendelea kuonesha ubora ambao ameuonesha katika michezo hii ya kujiandaa na msimu mpya ni wazi kiungo atarudisha nafasi yake kwenye kikosi cha Real Madrid kama ambavyo alikua akipata mwanzoni mwa msimu uliomalizika.TchouameniKlabu ya Real Madrid wana utajiri wa viungo wa katikati lakini hawana kiungo mwenye uwezo kukaba na kushambulia, Hivo kukosekana ndani ya kikosi hicho kulikua kuna kitu kinakosekana kitu ambacho kinaonekana kwasasa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa