Rais wa La Liga Javier Tebas amesama ana ushahidi wa kuthibitisha kuwa Paris Saint Germain wamekuwa wakitumia udanganyifu kukwepa sheria ya matumizi mabaya ya fedha “Financial Fair Play regulations.”
Tebas amekuwa akiikosoa PSG mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni na kuiita Ligue 1 “adui” baada ya Messi kuhamia Ufaransa kwa uhamisho huru.

Tebas amekuwa akiendeleza vita ya maneno na klabu hiyo ya Ufaransa leo alipokuwa akifanya mahojiano na L’Equipe, aliwatuhumu tena kwa kutumia pesa nyingi kuliko wanazoingiza.
“Naweza kukuonyesha jinsi wanavyo danganya kwenye haki ya matumizi ya pesa, kabla ya Messi, PSG walikuwa waningiza asilimia 40 ya mapato kupitia udhamini.
“Kama Messi na Neymar wakibaki mie sijari, ila hii inaumiza vilabu vingi vya ulaya, sipo peke yangu mimayesama, nawakosoa sababu hawawezi kulipa wachezaji kwa pesa walizonazo, hii inaondoa ushinadani.
“Wanawezaje kuwa na kikosi chenye thamani ya karibia €600m, wakati wakichukua ubingwa wa ligue 1 , hawawezi kuingia hata €45m, hii haiwezekani, ila wao ni wepesi kunikosoa mimi ,lakini hawana majibu.”
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


