Deontay Wilder amesema kwamba yupo sawa kumkabili mpinzani wake Tyson Fury na adai kwamba sasa hivi ameimarika tangu alipopigwa katika pambano lao la pili na Mmarekani safari hii anataka kulipa kisasi huko Las Vegas Wikendi hii.

“Najiona nikimpiga na kisha kumdondosha, niliona vitu vingi kwenye pambano la kwanza na la pili lakini sikutekeleza mpango wa mechi. Lakini safari hii nina hisia tofauti, Nguvu niliyonayo sasa hakika naangalia mbele na kuwekeza akili kwenye pambano la Okatoba 9.” alisema Deontay Wilder.
Tyson Fury alimwita Wilder ‘Takataka’ kuelekea pambano lao la tatu “Katika pambano la kwanza Wilder alikuwa kipigana kwaajili ya familia yake kwaajili ya watoto wake. Lakini kwa sasa ni takataka tu, nakwenda kumdunda tena siku ya Jumamosi usiku,” alisema Tyson Fury
Pambano la Fury vs Wilder 3 litafanyika siku ya Jumamosi usiku huko Las Vegas nchini Marekani.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


