Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema suala la klabu yake kushinda mataji manne msimu huu ni suala ambalo linazungmwa na mashabiki wa klabu hiyo tu.
Erik Ten Hag anasema kua kumekua na maneno mengi juu ya Man United kushinda mataji manne kwenye msimu mmoja, Lakini kocha huyo anasema sio suala ambalo amelipa nafasi kwenye akili yake na sasa na hilo ni suala ameliacha kwa mashabiki wa klabu hiyo ila kwa upande wao halipo.Klabu ya Manchester United mpaka sasa ni klabu pekee kutoka ligi kuu ya Uingereza ambayo inashiriki michuano yote mpaka sasa, Huku ikifanikiwa kushinda taji moja la Carabao Cup na kubakiza mataji matatu yaliobaki na mpaka sasa wapo kwenye kinyang’anyiro cha mataji yote matatu.
Kocha Ten Hag wakati anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya West Ham kwenye kombe la FA, Akionekana ni kama amepinga kauli ya mchezaji wake Wout Weghorst ambaye alisema wako kwenye mipango ya kushinda mataji manne msimu huu.Baada ya kocha Ten Hag kuzungumza kua suala la kushinda mataji manne msimu huu halipo kwenye akili yake, Lakini wengine wametafsiri ni kama kocha anacheza na akili ya makocha wengine kwani klabu hiyo inashiriki michuano yote na inafukuzia mataji yote matatu yaliyobakia.