Klabu ya Manchester United inaripotiwa kuwa imempa ofa ya mkataba wa miaka mitano  staa wa Real Madrid Raphael Varane, katika jitihada za kumshawishi kuhamia klabuni hapo.

Mlinzi huyu kwa sasa yupo katika majukumu ya kitaifa na kikosi chake cha Ufaransa katika maandalizi ya Euro 2021, akiwa amesalia na mwaka mmoja tu kwenye makataba wake wa sasa na Real Madrid.

Man United wanaendelea kuhusishwa kwa ukaribu zaidi na Varane mshindi wa Kombe la Dunia, huku Chelsea, Manchester City na Liverpool wakitajwa kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa hali ya mkataba wake.

Kwa mujibu wa chapisho la ABC, miamba hawa wa Uingereza wametoa ofa bomba ya mkataba wa miaka 5, japokuwa bado haijafanya makubaliano rasmi na Real Madrid juu ya gharama za uhamisho.

Mitano Tena kwa Raphael Varane Madrid au United?

Ripoti zinasema kuwa Real Madrid wanaweza kumuacha Raphael Varane aondoke, lakini hawatakuwa tayari kupokea kiasi chochote chini ya €70m (£60.2m) kwa sababu ya umuhimu wake kikosini.

Kwa upande wa Varane, yeye anasema kuwa kwa sasa anazingatia majukumu aliyonayo kitaifa, na baada ya hapo atakuwa tayari kuzungumza na klabu juu ya hatma yake.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa