Rafael Nadal Bingwa wa French Open 2020.

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Rafael Nadal ameifikia rekodi ya Rodger Federer kwa kutwaa taji la 20 la Grand Slam na kuweka rekodi ya kubeba taji la French Open mara 13.

Nadal ameumaliza mwendo katika namna ya aina yake baada ya kumlaza na viatu mpinzani wake Novak Djokovic kwa ushindi wa seti  6-0 6-2 7-5 katika mchezo wa Fainali ya French Open 2020.

Huu ni mchezo wa kwanza 2020 kwa Djokovic kupoteza. Baadhi ya wapenzi wa mchezo wa tenesi walijaribu kuhoji kiwango cha Rafael Nadal akiwa na umri wa 34, jibu la Nadal lilionekana dhahiri uwanjani kwa kuonesha kiwango cha hali ya juu.

 

Rafael Nadal akishangilia ushindi wa French Open 2020

Mchezo uliotumia muda wa saa2 na dakika 41, Nadal alionesha umahiri wake wa kupiga mipira mirefu na kujibu mashambulizi ya Djokovic, hata hivyo mipira yenye kasi kubwa kutoka kwa Rafael Nadal ilikuwa ni changamoto kwa Djokovic.

Ushindi huu unampa nafasi Nadal kupambana na Rodger Federer katika kumpata bingwa wa muda wote kwenye ulimwengu wa tenesi kwa wanaume duniani. Mpaka sasa, Nadal na Federer wanaidadi sawa ya mataji (20) huku Djokovic akiwa na mataji 17.

“Huu ushindi una maana kubwa sana kwangu. Kiukweli sifikirii sana taji la 20 la Grand Slam na kumfikia Federer, kwangu mimi ni ushindi Roland Garros.

“Kucheza hapa ni hamasa kubwa na mapenzi yangu kwa mji na uwanja huu, hayatosahaulika.” alisema Nadal baada ya mchezo wa fainali.

Mbio za kumtafuta Bingwa wa Dunia mwenye mataji mengi ya Grand Slam
Zifahamu takwimu za kipekee za Rafael Nadal kwenye Roland Garros.

13 – Hakuna mchezaji yeyote aliyeshinda mataji mengi ya Grand Slam sehemu moja.

15 – imeshapita miaka 15 tangu abebe taji lake la kwanza la Grand Slam, Serena Williams pekee ndiye aliyemzidi katika hili.

100 – Nadal ndio mchezaji pekee aliyeshinda mechi nyingi za Roland Garros.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

13 Komentara

    safi sana rafael umejituma sana na umepata ulichokuwa unahitaji

    Jibu

    Safi sana ubingwa ulikuwa wako huo

    Jibu

    Pongezi zake Nadal

    Jibu

    Kuluka luka kwake djokovic lakini haikufua dafu kwa nadal mwisho wa siku kaangukia kisiki tumeona kazi ya djokovic amejituma sana kwa matokea aliyokua nayo ilionesha zaili kabic ushindi ulikua wake..! Pongezi sana nadal ila usilewe sifa bado hana safari ndefu

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Pongezi zake Nadal

    Jibu

    Pongezi kwake rafael

    Jibu

    Amewek record nzur

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Hongera sana Rafael

    Jibu

    Big up sana kijana

    Jibu

    Good news

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.