Mcheza tennis kutoka nchini Serbia Novak Djokovic ameshinda taji lake la saba la mashindandano ya Wimbledon ambayo yanafanyika nchini Uingereza kwa kumchapa mcheza tennis kutoka nchini Australia Nick Kyrgios.

Djokovic alitumia utulivu mkubwa dhidi ya Nick Kyrgios ili kufanikiwa kumshinda kwenye mashindano hayo. Mserbia huyo ameshinda mara nne kwenye michuano ya uwanja wa nyasi katila Grand Slam.

Novak Djokovic, Novak Djokovic Ashinda Taji Lake la Saba la Wimbledon, Meridianbet

Novak Djokovic alifanikiwa kushinda kwa set 4-6, 6-3, 6-4, 7-6. Djokovic anakuwa mcheza tennis namba mbili kutokupoteza mchezo kwenye uwanja wa wimbledon, huku namba moja ikishikiliwa na Roger Federer.

“Nimekosa maneno katika michuanono hii na ushindi huu una maana kubwa kwangu, mara zote imekuwa hivyo na itakuwa michuano maalum kwenye moyo wangu.

“Imenihamishia mimi kuanza kucheza tenesi, kila muda mashindano haya yanazidi kuwa na maana na maalum.” Novak Djokovic alinukuliwa akisema baada ya mchezo kuisha.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa