Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema Mkufunzi wa Barcelona Ronald Koeman bado ana matumaini kwamba Lionel Messi atasalia katika klabu hiyo na kukataa kuingizwa katika mjadala kuhusu hatma ya baadae ya nyota huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33.

Tottenham huenda ikawasajili wachezaji zaidi mwezi Januari na inatarajiwa kumtafuta mlinzi mpya wa safu ya kati, huku mchezaji wa kimataifa wa Colombia Davinson Sanchez, 24, akitarajiwa kuondoka.

Kiungo wa kati wa Mbrazil Willian, 32, ‘amechukuliwa hatua’ na Arsenal baada ya kwenda Dubai wiki kadhaa zilizopita – huku Mikel Arteta akisisitiza suala hilo ‘limesuluhishwa’.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Jurgen Klopp anasisitiza kuwa hana habari kuwa mabingwa wa Ligi ya Premia Liverpool, wanapania kumnunua mlinzi mpya mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.

Liverpool wamefahamishwa kuwa watalazimika kulipa £26.7m ikiwa wanamtaka mlinzi wa Ajax Perr Schuurs, 20, huku AC Milan pia wakionesha nia ya kutaka kumnunua mholanzi huyo anayecheza safu ya kati na nyuma.

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti amepuuzilia mbali tetesi zinazoashiria anawataka wachezaji wake wawili wa zamani; kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Isco, 28, na kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Sami Khedira, 33.

Tetesi zinasema West Ham pia wamehusishwa na mshindi wa zamani wa Kombe la Dunia Khedira.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 28, hana mpango wa kuondoka Arsenal kuelekea Inter Milan mwezi Januari.

Baba yake Erling Haaland, Alf-Inge, kiungo wa kati wa Nottingham Forest, Leeds na Manchester City, amekiri kuwa mwanawe ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Norway, 20, anatamani kujiunga Ligi ya Premier lakini kwanza anataka kushinda taji na klabu yake ya sasa, Borussia Dortmund.

Kiungio wa kati wa zamani wa Manchester City Trevor Sinclair, anaamini kuwasili kwa mchezaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, 33, ‘hakutaepukika’ baada ya mkataba wa mkufunzi wa City Pep Guardiola kurefushwa.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

17 Komentara

    barcelona wamuache messi ndo awe muamuzi wa maisha yake ya soka

    Jibu

    Messi ndiyo Kila kitu Barcelona

    Jibu

    Yani Barcelona bado Wana umizwa vichwa na Messi ivi Messi akitoka apo Barcelona kutakuwaje Barcelona ataweza kuendeshwa au ndompaka Messi awepo mwacheni tuu nayeye akangalie soka kwingine

    Jibu

    Messi roho yake haitaki kubaki Barca

    Jibu

    Messi kam kashachoka barcelona wamuache tyu afanye maamuz yake!

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Makala bomba!!!

    Jibu

    Dilisha la usajiri likifunguliwa sizani kama man u watakaa nyuma tena

    Jibu

    Haya kaz kwao

    Jibu

    Messi kwa gunzo

    Jibu

    Thanks for new updates.

    Jibu

    Good news

    Jibu

    habari njema

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Mess yupo vizuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.